0

  MBUNGE WA JIMBO LA RORYA LAMECK AIRO AMETOA MISAADA YA MIPIRA KWA  TIMU YA SOKA YA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KUJIANDAA NA MCHEZO WA NA  TIMU YA WAKUSANYA KODI WA TRA HAPO KESHO

MSHAMBULIAJI WA TIMU YA WANA HABARI MARA AUGUSTINE MGENDI ANAYEANGALIA KAMERA AKISUBILI KUANZA KWA MAZOEZI YA MAANDALIZI HAPO JANA
                                         Majadiliano muhimu kabala ya kuanza mazoezi sikuwa kimazoezi ki vile
     Mmoja wa Mackocha mkoani Mara wanaotumia muda wao kukuza vipaji,Mwl Matitu aitabilia ushindi timu ya wana habari mara
lazima afe mtu
                                           Jamaa wakijadili juu ya mechi hiyoooooooooo
                                                  Mchezaji wa timu ya wanahabari Mara,Mwl Luhende
                     Mchezaji tegemeo wa TRA  Mara akijiuliza kama ataweza mziki wa wanahabari
 
                 Du Mpira c Maneno bali ni vitendooooooooooooo

                       KWA MAZOEZI HAYA HAWATOKI
                                      Mazoezi ya Viungo Muhimu katika kuweka Mwili sawa
                                     kocha mchezaji wa TRA MARA

                       
Amani Richard pamoja na Martini Mumbala wakijiandaa kufanya Mazozi   ikiwa ni Maandalizi ya Mchezo kati ya Timu ya waandishi wa habari Mkoani Mara na Wakusanya Mapato TRA na hawa ni miongoni mwa wachezaji wa TRA walionunuliwa kwa ajili ya mchezo huo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo ameipa misaada ya mipira miwili timu ya soka ya waandishi wa Habari Mara ikiwa ni kutoa hamasa ili kuweza kuafanya vizuri katika mchezo wao na timu ya wakusanya ushuru wa timu ya TRA Mara katika maazimisho ya wiki ya mlipa kodi hapo kesho.

Akikabidhi mipra miwili kwa ajili ya ya mchezo huo ambao umejaa kila maneno ya tambo kutoka kwa timu zote,Lameck amesema msaada huo ni misehemu ya misaada mbalimbali ya vifaa vya michezo ambavyo amepanga kuisaidia timu hiyo katika kuijenga na kuifanya kuwa timu ya kudumu.

Amesema kuwa waandishi wa Habari wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika jamii katika kuifahamisha masuala mbalimbali hivyo kama wameamua kuunda na kuwa na timu ya michezo kila mdau anapaswa kuisaidia ili waendelee kujenga afya kupitia michezo na kuendelea kuipasha jamii habari.

Lameck amesema licha ya kutoa mipira hiyo ataendelea kutoa misaada mingine ya michezo kwa timu hiyo ya wana habari zikiwemo jezi na vifaa vingine ili kuifanya kuwa ni moja ya timu kubwa na si tu Mkoa wa Mara bali na katika medani nyingine za michezo.

Nahodha msaidizi wa timu ya Waandishi wa Habari Mara Augustine Mgendi amemshukuru Mbunge huyo wa Jimbo la Rorya kwa msaada huo na kudai kuwa itakuwa chachu ya kuhakikisha kesho wanafundisha mbinu za kukusanya kodi Maafisa wa TRA katika mchezo huo ambao ni maarum katika kuhamasisha ulipaji kodi.

Binda amesema wachezaji wote wa timu ya Waandishi wa Habari wapo fit kwa ajili ya mchezo huo na hawaogopI majingambo ambayo yamekuwa yakitolewa mtaani na timu ya wakusanya mapato wa TRA kwani kikosi chao kimefanya mazoezi ya kutosha chini ya wachezaji wao hatari kama George Marato,Thomas Dominick,Emanuel Amas na wengineo.

Mchezo wa kati ya Waandishi wa Habari Mara na wafanyakazi wa TRA utafanyika katika viwanja vya Posta Mjini Musoma huku mashabiki wa soka wakiombwa kijitokeza kwa wingi ili kupata burudani kwani hakutakuwa na kiingilio chochote.    

Post a Comment