0
shuka chini kwa picha na maelezo zaidi
George Marato wa ITV akimuhoji kamanda Mwakyoma
nnjini zilizokamatwa na Jeshi la Polisi pamoja na majambazi
mkuu wa upepelezi afande Mahamud huku kushoto kwake akiwepo mkuu wa kituo mjini Musoma afande Hupa wakifatilia kwa karibu maelezo ya Kamanda Mwakyoma
Mpiga picha wa itv maxmilian Dominick akitafuta picha nzuri kwa ajili ya habari
Na Shomari Binda
        Musoma,

Jeshi la Polisi Mkoani Mara linawashikilia watu tisa wanaodaiwa kujihusisha na ujambazi katika Ziwa Victoria kwa kuwanyang'anya Wavuvi mali zao zikiwemo boti, njini,pesa pamoja na vifaa vingine wanavyovitumia wakati wa uvuvi na kisha kuwatosa majini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake,Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma alisema kukamatwa kwa majambazi hayo kunatokana na ushirikiano ambao wameupata kutoka kwa Raia wema kutokana na kuchoshwa na vitendo ambavyo imekuwa vikitendeka kwa wavuvi.

Katika tukio lingine Kamanda Mwakyoma alisema Mahabusu mmoja Wilayani Serengeti anayetuhumiwa kwa wizi wa baiskeli Nichoilaus Magesa alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na askari Polisi baada ya kutaka kutoroka akiwa njiani kurejeshwa gerezani  na kulazwa katika Hospitali ya DDH Wilaya Bunda

Kamanda Mwakyoma alisema Mnamo Novemba 21 Mwaka huu majira ya saa za usiku katika Kisiwa cha Rukuba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara Wavuvi watatu Nyantora Nyihande (42),Mwita Nyamsya (35) na Nyaganga Tibe wa kambi ya uvuvi Elikana katika kisiwa hicho wakiwa katika shughuli zao za uvuvi walivamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kuwavua nguo na kuwanyang'anya njini pamoja na boti.

Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo,Jeshi la Polisi liliamua kuendesha Operesheni isiyokoma katika ziwa Victoria na kufanikiwa kuwakamata majambazi hayo ambapo wengine wamekili kuhusika na vitendo hivyo ambavyo vikekuwa vikitokea mara kwa mara katika ziwa hilo.

"Hawa tumefanikiwa kuwakamata lakini sio kwa juhudi za Polisi pekee pia Raia wema wametusaidia sana katika operesheni hii ambayo imezaa matunda kwa kufanikiwa kuwatia nguvuni wanyang'anyi hawa ambao wamekwa wakiwakosesha amani wavuvi wanapokuwa katika shughuli zao za uvuvi.

"Nipende kuwahakikishia Waandishi wa Habari ya kwamba operesheni hii haitakoma itaendelea kufanyika kwa wakati wote ili kuhakikisha vitendo vya uhalifu ndani ya ziwa Victoria vinakomeshwa kwa kuwatia nguvuni wale wote wanaohusika na vitendo hivi.

Alisema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata njini nne za boti ambazo walinyang'anywa wavuvi walipoikuwa katika shughuli zao za uvuvi na kuwaomba Wananchi ambao walichuliwa mashine zao na wana vielelezo waende katika kituo kikuu cha Polisi Mjini Musoma ili waweze kizitambua.

Kamanda Mwakyoma aliwataja majamabazi hayo amabayo yanashikiliwa na Jeshi la Polisi kabla ya kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika kuwa ni Musa Ismail Matara mkazi wa Nyakato Mjini Msoma,Osunga Kiti,Otieno Zacharia,Guya Odudo Ayadu na Zuberi Christopher wakazi wa Rorya.

Wengine waliokamatwa kuhusiana na matukio ya unyang'anyia katika ziwa Victoria ni pamoja na Charles Nyaseri,Javen Baraka,Pamela Nyaumo na Nyambarya Matara ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika matukio hayo.

Aidha Kamanda Mwakyoma amewaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwatia nguvuni wale wote wanaodaiwa kujihusisha katika vitendo vya uhalifu kwa kusema kazi hiyo haiwezi kufanywa na Polisi pkee yao bali kila mmoja analo jukumu la kuhakikisha hali ya usalama katika jamii inakuwepo.

Post a Comment