0
WADAU WA DASIP WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MKUTANO AFRUX HOTEL

MGENI RASMI Eng.MATHAYO ATHUMANI AKIFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA DASIP








MWANDISHI MWANDAMIZI WA ITV GEORGE MARATO AKIFANYA MAHOJIANO NA MKUU WA MAFUNZO WA DASIP JULIUS SOKONO
Na Shomari Binda
        Musoma,

JUMLA ya masoko saba ya kisasa ya mazao ya kilimo na mifugo  yatakayoghalimu kiasi cha  zaidi ya shilingi bilioni 3.5 yanatarajiwa kujengwa na benki ya Maendeleo Barani Afrika (ADB) katika Wilaya sita zinazopakana nanchi jirani za Kenya na Uganda.


Ujenzi huo unalenga kutatua changamoto kubwa ya ukosefu wa masoko ya mazao inayowakabili wakulima na wafugaji katika maeneo hayo.

Mkuu wa mafunzo wa  Mradi wa Uwekezaji katika kilimo Wilayani (DASIP) kanda ya ziwa Julius Sokono aliyasema hayo juzi mjini hapa katika mkutano ambao umeshirikisha watalaam wa sekta kilimo na mifugo kutoka halmashauri 28 za mikoa ya Mara,Kagera,Kigoma,Shinyanga na Mwanza.

Alisema mchakato wa ujenzi wa masoko hayo ambalo kila moja linatarajia kugharimu milioni 500 umeanza kwa kuhusisha wilaya za Tarime (Mara) Ngara,Karagwe,misenyi(Kagera na Kahama (Shinyanga) pamoja na Kasulu mkoani Kigoma umeanza huku jamii ikitakiwa kuchangia asilimia 20  za mradi.

“Tayari mchakato wa ujenzi wa masoko hayo ya kati huko katika hatua za mwisho kwa kutangaza zabuni za ujenzi sisi dasip ambao ndio tunasimamia ujenzi huu tunaamini kuwa kukamilika kwa ujenzi huu kutafungua fursa kwa wafugaji na wakulima kupata soko la uhakika jambo litalowawezesha kujiongezea kipato na kupunguza umasikini”alisema

Alisema mradi wa dasip  ambao ndio unasimamia ujenzi wa masoko hayo,tayari umetekeleza miradi zaidi ya 2500 na kuunda vikundi 11,375 katika vijiji 780 vya halmashauri  28 katika mikoa hiyo mitano,lengo likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo na kukuza kipato cha wananchi walio ndani ya mradi

“Kupitia (DASIP) wakulima na wafugaji 252,836 wamepatiwa mafunzo mbalimbali  yakihusisha vijiji hivi 780 vya katika halmashauri 28 nchini yaliyohusu kanuni za msingi za uzalishaji wa mazao,ufugaji wa kuku na mbuzi pamoja na kuwezeshwa kuunda vikundi hivyo 11,375  vikiwa katika eneo ya mradi”alisema.

Alisema wakulima hao pia wameweza kunufaika na mafunzo ujasilimali,matumizi bora ya mbolea na udhibiti wa wadudu na magonjwa kupitia mashamba darasa wanatoka katika halmashauri hizo za mikoa ya hiyo ya Mara,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Mwanza.

Sonoko alisema pamoja na mafunzo hayo Dasip kati ya miradi hiyo zaidi ya 2500 ambayo imetekelezwa na Dasip katika vijiji hivyo  205 ni majosho ya kuogeshea mifugo,masoko 150,malambo ya maji 160,maghala ya vyakula 162 na miradi ya midogo ya umwagiliaji 34.

Aliongeza kuwa kupitia vikundi hivyo wakulima wameweza kupanunuliwa mashine za kusaga 440,trekta ndogo za kulimia power tillers 350 pamoja na mashine 36 za kuchakata mihogo ambayo imesaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo sambamba na kuongeza kipato kwa wananchi.

Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Mara,Mhandisi wa Maji Mkoa Eng Mathayo Athuman,aliwataka wataalam hao kutumia mkutano huo kuweka mipango ya kuwezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili sektsa ya kilimo na ufugaji ili kuleta mabadiliko yenye tija kwa wakulima na wafugaji katika maeneo yao.
Alisisitiza wataalam hao kutumia mafunzo hayo pia kukabiliana na changamoto ambazo zimesabisha miradi mingi ambayo imejengwa kupitia chini ya Dasip kuwa chini ya kiwango huku mingine kushindwa kutumika hadi sasa.

“Ni lazima tujue kuwa serikali yetu haiwezi kuendelea kukopa fedha na sisi kama viongozi wa umma tukaziacha zikapotea na wananchi wakaendelea kuteseka na baadaye wakalipa mikopo ambayo haikuwanufaisha”alisisitiza katibu tawala mkoa wa Mara katika hotuba yake hiyo.

Post a Comment