0
WANAFUNZI WA CLUB ZA WAPINGA RUSHWA KUTOKA SHULE YA SEKONDARI SONGE NA MUSOMA TEC NAO WALIKUWEPO KATIKA KUPELEKA MISAADA HIYO
NAIBU MKUU WA TAKUKURU MARA YUSTINA CHAGAKA AKIMKABIDHI SEHEMU YA MSAADA PADRI BISEKO
SEHEMY YA MISAADA ILIYOPELEKWA MJI WA HURUMA
WATU WENYE UHITAJI WANAOLELEWA KATIKA KITUO HICHO
BAADHI YA MAAFISA WA TAKUKURU MARA WALIOFIKA KITUONI HAPO
PADRI GODFREY BISEKO AKIAAGANA NA MAAFISA WA TAKUKURU
NAIBU TAKUKURU MARA AKIAGANA NA PADRI BISEKO
FRENK NAE HAKUWA MBALI
  Na Shomari Binda
         Musoma,

IMEDAIWA jamii kutokuwa na maadili inapelekea kuendelea kuwa na tatizo kubwa la kupambana na vitendo vya Rushwa hali inayopelekea kutokupatikana  haki katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Mlezi wa kituo cha Mji wa Huruma kinachowalea watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo walemavu,wazee na wale wenye upungufu wa akili Padri Godfrey Biseko wakati akipokea misaada ya mahindi,mafuta ya kula,sabuni,maharagwe,sukari pamoja na mafuta ya ngozi kutoka taasissi ya kuzui na kupambana na Rushwa Mkoani mara Takukuru.

Alisema Jamii imeondokana na maadili kwa kufanya vitendo visivyofaa vya ukiukwaji wa maadili na kujiiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinapelekea vichocheo vya kuomba na kupoke Rushwa hivyo haki kushindwa kupatikana na kudai kuwa maandiko matakatifu yanamtaka kila mwanadamu kualinda maadili.

Padri Biseko alidai katika Jamii maadili yameondoka huku baadhi ya Jamii ikiwatekeleza ndugu zao ambao wamekuwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ulemavu wa akili hali inayopelekea kuangaika mitaani kana kana kwamba hawana ndugu ambao wanaweza kuwalea na kuwatunza.

Alisema katika kituo cha Mji wa Huruma watu wanaowalea ni pamoja na waliowakuta mitaani wakiwa wanaangaika na kubezwa na kuamua kuwachukua na kuwaweka katika kituo hicho huku wakiwahudumia mahitaji mbalimbali ya kijamii anayohitaji mwanadamu.

"Kwa kweli maadili yameondoka katika jamii mtu anadiliki kufanya mapenzi na mtu mwenye upungufu wa akili na kumpa ujauzito hali yakuwa anajua ataangaika katika malezi ya mtoto atakaye jifungua tutaendelea kufanya maombi ili jamii iweze kubadilika na kumrudia Mungu,"alisema Padri Biseko.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoani Mara Yustina Chagaka alisema katika maazimisho ya siku ya Kimataifa ya Kuzui na Kupambana na Rushwa Takukuru kwa kushirikiana na vilabu vya wapinga Rushwa wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti,kutembelea wagonjwa,kufanya usafi,kutembelea vituo vya Watoto yatima pamoja na kuendesha mijadala ya wazi na midahalo.

Alisema lengo la kuazishwa kwa siku hiyo ni kuimalisha,kukuza na kusisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia maadili katika kuzuia na kupambana na Rushwa pamoja na wadau wote kubaini madhara ya Rushwa na namna ya kuikabili.

Hata hivyo alidai ni wajibu wa wadau wote kutambua mafanikio ya mapambano hayo,changamoto zilizopo ,kupanga mikakati na kutathimini ushiriki wa Tanzania katika mapambano Kimataifa.

Takukuru Mkoani Mara katika madhimisho ya Mwaka huu imetoa misaada yenye thamnai ya shilingi laki sita katiuka Kituo hicho cha Mji wa Huruma kilichopo maeneo ya Mkoko nje kidogo ya Mji wa Musoma na kutoa wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema kujitoa kusaidia watu wenye uhitaji kote Nchini ikiwa ni pamoja na kituo cha Mji wa Huruma.


Post a Comment