0
WANANCHI WAKIFATILIA KWA UMAKINI MKUTANO


POWWWWWWWWWWWWWWWER,NI KAMA WANAITIKIA

NYERERE AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO HUO

NAYE HAYUKO NYUMA

NYERERE AKIWA NA LEMA

LEMA NYERERE JUKWAANI




MAARUFU SANA KWA JINA LA JUGUNUU KATIKATI ALIYEKUWA MWENEZI WA KATA YA MWIGOBERO CCM AMBAYE ALITANGAZA KUHAMIA RASMI CHADEMA

MZEE MASAWE MAARUFU MJINI MUSOMA AKIWA NA LEMA

NAMBA PIA ZILIKUWA NA UMUHIMU WAKE


JIONI SANA BAADA YA MKUTANO WAKEREKETWA WALIWASINDIKIZA VIONGOZI HADI OFISINI  

     Na Shomari Binda
             Musoma,

MAELFU ya Wananchi wa Jimbo la Musoma na maeneo mbalimbali yanayozunguka Mji huo jana walijitokeza kwa wingi kuwasikiliza wanasiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo wakiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimboi la Arusha Mjini Godbles Lema na Mbunge wa Jimbo Hilo Visenti Nyerere.

Katika Mkutano huo ambao ulimalizika kwa Wananchi kuwasindikiza kwa msururu Mkubwa kutoka katika viwanja hivyo hadi katika makao makuu ya Chama hicho Wilaya ya Musoma Mjini kwa nyakati tofauti wanasiasa hao walitumia jukwaa kulaani matukio ambayo yamekuwa yakitokea yakiwemo ya mauaji.

Awali Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini Visenti Nyerere alitumia jukwaa hilo kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya kushindwa kufika katika mkutano huo licha ya kualikwa kutoa ufafanuzi kwa Wananchi kutokana na matukio mbalimbali ya mauaji ambayo yamekuwa yakitangazwa na yeye kukanusha.

"Akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya tumemualika kuja kutoa ufafanuzi kwa Wananchi juu ya yale yanayoelezwa lakini ameshindwa kufika na matokeo yake anatutumia ujumbe kwa njia ya simu akisema yupo kwenye sherehe za miaka 51 ya Uhuru huu si uungwana na tunasema yeye ameshindwa kuja tukisikia mtu mwingine amekufa tutaandamana kushinikiza aondoshwe katika Wilaya hii.

"Sisi hatutaki kujua idadi ya watu waliofikwa na matukio ya kuchinjwa hata kama amechinjwa mtu mmoja suala ni kutokea kwa tukio hilo hivyo akiwa kama mkuu wa Amani katika Wilaya alipaswa kuitika wito wa Mkutano huu na kuwaondoa hofu Wananchi kutokana na yale yaliyoelezwa",alisema Nyerere

Alisema suala hilo halikuwafurahisha lakini pia Mbunge huyo akamtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma kukatisha likizo yake ili kuja kutoa ushirikiano katika kukabiliana na matatizo yaliyojitokeza katika siku za hivi karibuni hali iliyopelekea Wananchi kuwa na hofu na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Akizungumzia suala la Maendeleo Nyerere alisema akiwa kama Mbunge kwa kushirikiana na Balaza la Madiwa linaloongozwa na Chadema watahakikisha yale yote waliyoyaleza katika kipindi cha kampeni yanatekelezwa nakuomba Wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kufanikisha.

"Wananchi wenyewe mnaona kwa kipindi cha muda mfupi barabara nyingi ambazo zilikuwa hazipitiki lakini leo zinapitika na kufika katika maeneo mbali yaliyokuwa korofi na haya ni maeneo machache katika miundombinu lakini pia hata katika miradi mingine ikiwemo ya maji utekelezaji wake unafanyika.

"Tumepata Bilioni 13 kutoka benki ya Dunia katika miradi ya barabara tunawahahakishia Wananchi fedha hizi zitafanya kazi kama zilivyoelekeza na zipo barabara ambazo zitakuwa na kiwango cha lami na nyingine za kiwango cha changarawe na tunataka kufikia mwaka 2013 mwishoni kila barabara iweze kupitika.

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbles Lema yeye aliwataka Wananchi kutokuwa moyo wa uoga katika kudai haki zao za msingi na kutoa ushirikiano na kushirikiana na viongozi wa Chadema katika kutafuta mabadiliko na badala yake kukaa pembeni na kuanza kulalamikia kila wakati.

"Nimewapenda vijana wa Musoma nyie ni Jasiri kama walivyo vijana wa Arusha ambao kila kukicha wanatamani mabadiliko lakini naamini ipo siku itafika na kile tunachokitaka kitafanikiwa lakini nawaomba ondoeni moyo wa uoga jengeni ujasiri na shirikianeni na viongozi wenu katika kutaka kujikomboa.

"Haina maana kila wakati kukaa pembeni na kuanza kulalamika maana mabadiliko hayaji kwa kulalamika tujitoe na tushirikiane katika kufanikisha kile ambacho tumekuwa tukikitaka ili kila mmoja aweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika Nchi hii ambazo zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache",alisema Lema

Lema alisema kila mmoja kwa nafasi yake anao wajibu wa kuhakikisha analeta mabadiliko na sio kazi ya kuwaachia viongozi pekee yao katika kuyatafuta huku wengine wakikaa pembeni na kuanza kulalamika kwani malalamiko yao yatakuwa hayana maana katika kufikia malengo ambayo yanakusudiwa.

Post a Comment