0

  
Na Shomari Binda
       Rorya,

CHAMA kipya cha Upinzani Nchini Tanzania cha Alliance For Democtratic Change (ADC) kilichopata usajil wa kudumui mwaka jana kimeendelea kujiimalisha katika Wilaya za Mkoa wa Mara baada ya kufanya uchaguzi na kuunda safu nzima ya uongozi katika Wilaya ya Rorya ikiwa ni Wilaya ya pili kufanya hivyo katika Mkoa huo.

Katika Uchaguzi huo uliofanyika katika Kata ya Nyathorogo ulihudhuliwa na Wanachama zaidi ya mia moja wa Chama hicho pamoja na Wananchi na Viongozi wa Vyama vingine vya Siasa Wilayani Rorya ulishuhudia Erinesti Ojunga akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho Wilayani Rorya kwa kupigiwa kura zote 107 za ndiyo baada ya kukosa mpinzani katika nafasi hiyo.

Awali akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzu huo ambaye pia ni Kamishina wa Chama cha ADC Mkoa wa Mara Jumanne Magafu aliwataka Wanachama wa Chama hicho kuwa makini katika kuchagua viongozi ambao watafikisha malengo ya Chama katika kuwafikia Wananchi kama Katiba inavyoeleza.

Alisema lengo la kuanzinshwa kwa Chama hicho ni kuwa Viongozi kuwashilikisha Wananchi katika shughuli zote zikiwemo za kiuchumi,Kijamii,Elimu na na masuala yote ya Shughuli za Kimaendeleo na Uwajibikaji kwa Viongozi kwa Wananchi.

Magafu alidai katika Imani ya Chama cha ADC kifungu cha 1.1 (a) hadi (n) kinaelezea masuala mazima ya Uwajibikaji wa Kiongozi na Ushilikishwaji wa Wananchi katika masula mbalimbali ya Kijamii bila kumtenga mtu yoyote lakini pia Imani ya Chama hicho inamtambua Mwenyezi Mungu ikiwa ni kumtaka kiongozi na Mwanachama yeyote kufanya kazi za Chama kwa kumheshimu Mungu.

Katika muundo wa Uongozi wa Katiba ya Chama cha ADC Katibu wa Wilaya ya Rorya wa Chama hicho Aboum Thomas hakupigiwa kura katika Mkutano huo bali aliteuliwa na Uongozi wa Taifa huku pia Mkutano huo ukichagua safu nyingine za Uongozi ikiwemo Bodi ya Uongozi kwa mujibu wa Katiba. 

Wajumbe wa Bodi ya Uongozi wa Chama hicho iliyochaguliwa katika Mkutano huo ni pamoja na Dominikus Ong'ong'a,Abouk Odiero,Jenifa Kanar,Joyce Dede,Joshua Kanar,Rajabu Samson,Ayoo Ayoma, Deus Akoto,Frola Kura pamoja na Owe seda.

Katika Uchaguzi huo wa Chama cha ADC Wilaya ya Rorya pia ilichaguliwa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ambao pia ni Wakuu wa Idara ya Chama hicho ambapo katika Idara ya Ulinzi na Usalama alichaguliwa Ayoo Ayoma,Mipango na Uchaguzi Joshua Kanar,Siasa na Uenezi Deus Akoto,Fedha na Utawala Frola Kura huku Haki za Binadamu Akichaguliwa Owe Seda.

Kamati ya Usuruhishi ya Wilaya,Richard Jaoko alichaguliwa kama Mwenyekiti na Ernest Nyakani Katibu huku Wajumbe wa Mkutano huo  wakiwa ni Edward George,Benard Onene,Eliva Paulo pamoja Abrosi Onono.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanda waliochaguliwa katika Uchaguzi huo ni Joseph James,Paulo Aduongo,Janeth Kanar pamoja Frola Kura ambao wataiwakilisha Wilaya ya Rorya katika Mkutano Mkuu wa Kanda.

Mara baada ya Uchaguzi huo kukamilika na kuundwa kwa safu nzima ya Uongozi wa ADC katika Wilaya ya Rorya,Wajumbe pamoja na VIongozi wa Chama hicho waliomba Uongozi wa Chama hicho ngazi ya Taifa kufanya jitihada ya kuwatafutia usafiri ambao utawasaidia kukiimalisha na kufanya shughuli za Chama katika maeneo mbalimbali ya Vijiji vya Wilaya hiyo.

Nao baadhi ya Wanachi na Viongozi wa Vyama vingine vya Kisiasa walioalikwa katika Mkutano huo wa Uchaguzi wa Chama cha ADC walisema Katiba ya Chama hicho kama ilivyoelezwa na Kamishina wa Chama hicho Mkoa iwapo viongozi wataifata kitakuwa ni Chama cha mfano wa kuigwa katika Taifa hasa katika ukomo wa Uongozi.

"Kwa kweli nimeipenda Katiba ya ADC japo mimi nimealikwa ni Mwanachama wa (CCM) nimeisoma na iwapo Viongozi waliochaguliwa wataifuata Chama hiki kitaimalika sana hasa katika Wilaya hii ya Rorya ambayo baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa wanafanya kazi kwa masrahi yao binafsi badala ya Wanachi,"alisema Otieno Opiyo aliyejitambulisha kama Mwanachama wa CCM.

Tayari Chama cha ADC kimeshafanya uchaguzi katika Wilaya ya Tarime na hivi sasa Chama hicho kinajipanga kuendelea na ratiba za kufanya Uchaguzi katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mara na baada ya Rorya kitaelekea katika Wilaya za Butiama,Musoma Mjini,Serengeti na baadae Wilaya ya Bunda.

Post a Comment