0
WANAJESHI WA AFRIKA WAKIINGIA NCHINI MALI

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa Afrika, kinachojiunga na muungano wa wanajeshi wa kimataifa dhidi wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali, kiliwasili nchini humo usiku wa kuamkia leo.

Hali ya Mali inaendelea kudhihirika huku nchi baada ya nyingine zikiendelea kujitolea kutuma vikosi.

Inatumia ndege za kijeshi pamoja na vifaru ambavyo vinashambulia maeneo ya waasi hao kote Kaskazini mwa Mali na maeneo mengine ya jangwa la Sahara.

Ufaransa ilianza kwa kutuma wanajeshi zaidi ya miamoja Mali lakini siku kadhaa tu katika harakati hizo, ikaahidi kuongeza idadi hiyo hadi wanajeshi elfu mbili na miatano.

Katika tukio lengine, nchi kubwa zaidi Magharibi mwa Afrika Nigeria, nayo pia ikajitolea kutuma wanajeshi,miasita. Idadi hiyo sasa imeongezeka mara dufu.

Nchi za Magharibi sasa kila kukicha zinakumbana na wapiganaji wenye nguvu wa kiisilamu katika msitari wa mbele nchini Mali.

Lakini kupambana na wanamgambo sio kazi rahisi. Wanaelewa vyema maeneo ya jangwa kuliko wanajeshi wa kigeni.

Pia wana miungano kadhaa au kuungwa mkono na wapiganaji wengine upande wa pili wa jangwa katika miji mikuu ya nchi jirani.
    
chanzo BBC

Post a Comment