BAADHI YA WANAWAKE WAKIWA KATIKA UWAJIBIKAJI SEHEMU ZA MIGODINI |
Na Shomari Binda
Butiama,
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Wilaya ya Butiama (UWT) na
Diwani wa Kata ya Bwiregi Nyagheti Adam alisema katika ziara yake ya
kuwashukuru Wananchi wa Wilaya ya Butiama kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti
wao atakayoianza hivi karibuni moja ya mambo atakayofanya ni
kuwahimiza Wanawake kujikita katika shughuli za Ujasiliamali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za UWT,Nyagheti
alisema katika ziara hiyo ambayo atazunguka katika kata zote za Wilaya
ya Butiama akiambatana na walimu wa masuala ya ujasiliamali lengo kuu ni
kuwajengea uwezo Wanawake kujifunza elimu ya ujasiliamali ambayo ameona
ndio ukombozi wa Mwanamke.
Alisema kutokana na upungufu wa ajira hususani kwa maeneo ya
pembezoni hakuna budi elimu ya ujasiliamali ipate kuenezwa katika maeneo
ya Vijijini ambayo itamfanya Mwanamke aweze kujitambua na kuelewa dhana
nzima ya ujasiliamali ili uwe ni ukombozi kwa Mwanamke.
Nyagheti alisema Mwanamke ambaye atapata Elimu ya ujasiliamali anao
uwezo mkubwa wa kupambana na majukumu ya kifamilia pasipo kuwa tegemezi
na kuonekana mtu wa chini muda wote na kutegemea kila hitaji kumuomba
Mwanaume nyumbani ama kumsubili mwanaume hata kama ametoka hata akiwa na
hitaji la chumvi.
"Lizima Mwanamke aheshimike na hawezi kuheshimika kama ataendelea
kuwa katika hali duni na kushindwa kujifanyia mahitaji yake hata madogo
madogo,ntajitahidi kadri ya uwezo wangu kushirikiana na Wanawake
wenzangu katika kujitafutia Maendeleo kwa njia ya kufanya ujasiliamali.
"Katika ziara yangu ya kutembelea Kata za Wilaya nzima ya Butiama
nitakuwa na watu wa maendeleo ya Jamii pamoja na walimu wa masuala ya
ujasiliamali nikiwa na lengo mahususi la kuwafikishie elimu Wanawake ili
mwisho wa siku kila Mwanamke ambaye ajaajiliwa aweze kujiajili kupitia
ujasiliamali,"alisema Nyagheti.
Mwenyekiti huyo wa UWT alisema Wanawake wa Wilaya ya Butiama na
Kata ya Bwiregi wamempa heshima kubwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake na wale walioshirikiana pamoja na Wanaume katika Kata ya
Bwiregi kuwa Mwanamke pekee wa kuchaguliwa kama Diwani kati ya Kata 34
za Wilaya ya Butiama.
"Kwanza sina budi kusema Wanawake waliniunga mkono kwa asilia kubwa
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nilipokuwa nagombea Udiwani katika
Kata ya Bwiregi licha ya kuwa wapo Wanaume ambao pia waliniunga mkono
katika kinyang'anyiro kile na Upinzania ulikuwa mkubwa sana.
"Kwa kuzingatia imani waliyoijenga kwangu nami sintowaangusha bali
ntahakikisha najitahidi kila linalowezekana hasa kubwa ikiwa ni elimu ya
ujasiliamali na kupeana njia za kuwezeshana kutoka kwa walimu na
kujifunza sehemu mbalimbali ili mwisho wa siku kila mmoja awe na uchumi
mzuri na kuweza kuendesha maisha ya kila siku,"alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema ziara amepanga kuanzia katika Tarafa ya Nyanja na kisha
kumalizi katika Tarafa ya Kiagata na kudai kuwa licha kuambatana na
walimu wa masuala ya ujasiliamali pia ataongozana na Viongozi wa Chama
cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama na kuwaomba Wananchi kufika katika
mikutano yake kwani kutakuwa na faida kubwa watakayoipata.
"
Post a Comment
0 comments