0
                           

Na Mwandishi wa Blog hii
         Mara,

Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Mkoa wa Mara hukosa mapato kutokana na makusanyo ya samaki hasa dagaa wanaosafirishwa kwenda nchi  jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo,Kenya, Uganda,Msumbiji na Nchi za Umoja wa Kiarabu (UAE)

Imebainika kuwa Biashara ya usafirishaji wa bidhaa hiyo imekuwa ikifanywa bila kuzingatia taratibu sahihi za usafirishaji ikidaiwa zinafanyika ndani ya Nchi lakini tafiti iliyofanywa imedaiwa wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha kupeleka nje ya Nchi bila kufuata utaratibu wa kupeleka bidhaa nje ya Nchi.

Wananchi wa maeneo ya uvuvi wa maeneo ya Busekera,Kome,Iriga,Bwai pamoja na Rukuba wameieleza BLOG hii katika mahojiano kuwa wanashangaa TRA kuangalia maeneo mengine ya makusanyo na kuacha eneo hili ambalo wamedai likiangaliwa kwa umakini linaweza kuliingizia pato kubwa Taifa.

Jitihada za kukutana na Meneja wa TRA Mkoa wa Mara ili aweze kuzumzia suala hilo halikuweza kufanikiwa kwa muda licha ya kufuatwa Ofisini kwake na kuambiwa katoka na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi hakuweza kupatikana.   

Imeelezwa zaidi ya tani 10,000 za dagaa usafirishwa kila siku wakati wa msimu  na mfanyabiashara mwenye asili ya Asia ambapo amekuwa akiwatumia wakazi wa maeneo ya Visiwani kuwasafisha na kutumia chanja maalumu ya kuanika na kupakia samaki hao kwenye malori tayari kwa kusafirishwa.
 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bukumi,Chomya Ndege pamoja na wananchi wa kijiji cha Busekela walishindwa kusema juu ya tatizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa alipofanya ziara yake ya kikazi na kufanya Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Msingi Busekela kutokana na kubanana na ratiba.

Diwani huyo alilamikia mambo mengine yakiwemo ya ukahaba yaliyopo katika maeneo ya wavuvi ambapo masuala ya ufuska yamekuwa yakifanyika licha ya jitihada ya kudhibiti kufanywa na kushindwa kutokana na nguvu ndogo ya askari waliopo katika maeneo hayo.

Amezungumzia pia masuala yaUjambazi pamoja na Uvuvi Haramu na kuomba vyombo vinavyohusika katika kudhibiti masuala hayo viweze kufatilia na ktafuta njia sahihi ya kuweza kudhibiti hali hiyo.

Post a Comment