0
MWANAHABARI AUGUSTINE MGENDI WA CHANEL TEN AKIPATA UFAFANUZI KUTOKA KWA MENEJA MAHUSIANO WA MGODI WA NORTH MARA SELEMAN MONATA
UFAFANUZI ZAIDI KUTOKA KWA MTAALAM WA VISIMA JOHN MURRAY WA ABG

 Na Shomari Binda
         Tarime,

UONGOZI wa Mgodi wa Nyamongo North  Mara unaomilikiwa na African Barrick  Gold (ABG) umesema maji yanayohifadhiwa katika bwawa la kuhifadhi maji ya mabaki yatokayo kiwandani baada ya kuchenjua dhahabu "Tailings Storage Facility"(TSF)  hayana madhara yoyote kwa Binadamu wala wanyama wanaotumia maji hayo kama ilivyodaiwa.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya Wananchi wanaozunguka Mgodi huo kudai kuwa maji yanayotokana na mabaki ya kiwandani yana madhara ambayo yameshapelekea kufa kwa mifugo yao na kuwadhuru watu wanayoyatumia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari waliokwenda kutembelea maeneo ya mabwawa hayo yaliyochimbwa kando ya Mgodi huo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara Gary Chapman alisema baada ya kuwekewa zuio la kimazingira kutililisha maji yoyote yatokanayo na maeneo ya kiutendaji ya mgodi umepelekea mkusanyiko mkubwa wa maji kufikia 5'000,000 m3.

''Baraza la Taifa la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Wizara ya Nishati na Madini (MEM) yametimizwa kwa kiwango cha kuridhisha ili kuweza kuruhusu zuio hili kuondolewa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa kiwanda cha kusafisha na kutibu maji na ni matumaini yetu zuio hili litaondolewa mapema mwaka 2013.

"Ziada ya maji yaliyojikusanya katika maeneo mbalimbali Mgodini itasafishwa na kutibiwa kupitia katika mitambo ya kiwanda kipya na kuruhusiwa kutiririka katika mazingira kwa idhini ya kibali kitolewacho na Wizara ya Maji kupitia Ofisi za Mamlaka ya Usimamazi wa Bonde la Ziwa Victoria,"alisema Chapman.

Alisema sampuli za maji yanayopita katika maeneo ya mgodi zilichukuliwa na wataalam kwenda kufanyiwa uchunguzi na ilibainika kwamba maji hayo yalikuwa katika hali ya kuridhisha kimazingira na kulikuwa hakuna visumishi vyovyote kwa kuwa maji hayo kwa kiwango kikubwa yalitokana na mvua zilizokuwa zikinyesha katika kipindi cha miezi ya Novemba na Desemba mwaka jana.

Chapman alidai hata hivyo Mgodi huo umechukua hatua nyingine ya kujenga kizuizi kingine katika eneo la mteremko la bwawa la TSF ili kuhakikisha kiasi chochote cha maji kitakachovuka kingamizi la awali kinazuiwa.

 
Alisema kutokana na ongezeko kubwa la maji katika bwawa la TSF limekuwa likipelekea  kiasi kidogo cha maji kuzana na kutoka nje kupitia katika kuta za bwawa hilo na baadae kukingwa katika vizuizi maalum na kusukumwa kwa pampu na kurudishwa katika bwawa la TSF.

Aliongeza kuwa ziara liyofanywa na tarehe 20 Desemba na Mamalaka mbalimbali ilikuwa na lengo la kukagua na kuthibitisha tathimini tatu za kimazingira zilizofanywa kwqa lengo la upanuzi wa bwawa la TSF,ujenzi wa eneo la kulundika mawe pamoja na tanuri la kuchomea takataka.

"Moja ya mapendekezo yaliyotolewa awali kuhusiana na tathimini ya kimazingira na upanuzi wa bwawa la TSF ilihusu kubolesha kwa vizuizi na makingamizi ya maji na tayari michoro iliyoandaliwa na wataalam tayari imeshafikishwa kwa Mamlaka za Serikali.

Akizungumzia hali iliyodaiwa kuwa maji hayo yana madhara kwa Binadamu na Wanyama,Meneja Mahusiano wa Mgodi huo Suleiman Monota alisema maji hayo hayana madhara na wapo Binadamu na Wanyama wanayoyatumia na hakuna taarifa ambazo wamefikishiwa juu ya kudhurika kutokana na maji hayo.

Alisema bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo Wananchi kuendelea kujenga katika maeneo ya Mgodi licha ya kuwa tayari wameshalipwa kupisha maeneo hayo lakini bado wameendelea kukahidi na kukwamisha shughuli nyingine za mgodi huo.

Post a Comment