0
MAREHEMU DOCTA JOSEPH NYAMAGWIRA
DAKTARI Msaidizi Mkuu Daraja la kwanza wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,Joseph Nyamagirwa (59) amefariki Dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoa wa Mwanza kwa tatizo la uvimbe sehemu ya chini ya utumbo mpana.

Daktari huyo ameacha pengo kubwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kutokana na kuwa tegemeo kubwa hasa kwa kutibu watoto na wanawake pamoja na upasuaji ambapo kwa sasa hospitali hiyo inahitaji madaktari 12 na hivi sasa waliopo ni watatu tu.

 

Akitoa taarifa ya kifo hicho,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Iragi Ngerageza alisema kuwa Marehemu alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akilalamikia kuwa linauma ambapo Jan.8 Mwaka huu alifika Hospitalini hapa kwa matibabu ambayo iliwalazimu kumpeka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando na siku hiyo hiyo akifanyiwa upasuaji wa kina.

Alisema kuwa pamoja na jitihada za madaktari bingwa kuokoa maisha yake lakini hali yake iliendelea kuzorota na hatimaye mauti kumfika Jan. 14 mwaka huu asubuhi ambapo alikuwa amelazwa katika chumba cha upasuaji idara ya upasuaji (Surgical Department) chumba namba 6 C 607.


Alikielezea wasifu wa marehemu alisema kuwa ni Daktari pekee ambaye alikuwa akifanya kazi kwa kujituma na kwa bidii kubwa na hata kama yuko likizo ataitwa kufanya kazi atakuja haraka na kwa gharama zake kusaidia wagonjwa ambao wanakuwa na hali mbaya.


“Kwa kweli Mkoa wa Mara tumepata pengo kubwa kumpoteza ambapo marehemu aliitwa jina la utani la ‘Chief’kutokana na uchapakazi wake,alikuwa alikifanya kazi ya uhakika kwa kuwa alikuwa atayari na uzoefu wa muda mrefu na kila upasuaji unapofanyika lazima awepo akimabatana na jopo la madaktari wengine kusaidiana nao na hatimaye kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa akina Mama Wajawazito na Watoto”Alisema Ngerageza.


Aidha ametoa wito kwa Wizara ya afya kuangalia uwezekano wa kuleta madaktari kwani kuna aupungufu mkubwa ambapo kwa kwa upande wa madaktari bingwa wanahitajika sita waliopo ni wawili tu na madaktari wasaidizi wanahitajika 28 waliopo ni 16 wamebaki 15.

 

Akizungumzia elimu yake Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,Faustin Bigambo alisema,alimaliza elimu ya Sekondari mwaka 1976 katika Shule ya Sekondari ya Sengerema na kujiunga na Chuo cha Utabibu cha Tanga na baadae kujiendeleza katika Chuo cha Madaktari wasaidizi cha Bugando Mwanza(BMC).

Marehemu atazikwa Jan.17 mwaka huu kijijini kwao Butata Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara,ambapo Maziko hayo yanatarajiwa kuhuduhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Tuppa.


Post a Comment