0
   
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA



Na Shomari Binda
         Butiama,

WAZAZI na Walezi walio na Watoto wenye umri chini ya Miaka 5 wamehimizwa kuwapeleka katika vituo vya zahanati watoto wao kupata chanjo ili kuepukana na maradhi yanasosababisha vifo vingi vya watoto ili kufikia malengo ya melinia namba 4 ifikapo Mwaka 2015.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupp katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula kwa niaba yake katika uzinduzi wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kuhara na nimonia uliofanyika katika kata ya Kukirango  Wilayani Butiama na kuhudhuliwa na wataalamu wa afya na viongozi wa Serikali Mkoani Mara.

Alisema malengo ya melenia namba 4 na 5 ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia yanahusu kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa uzazi na watoto walio na umri chini ya miaka 5 ambavyo vimekuwa vikitokea kwa wingi na kupelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa.

Tuppa alisema malengo ya melenia na Mkukuta yaliyotafsiriwa katika Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) yamelenga kupunguza vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka 5 toka 81 vya sasa hadi 54 katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa na vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja toka 32 vya sasa hadi 19 kila watoto 1,000 waliozaliwa hai ifikapo Mwaka 2015.

Alisema idadi ya magonjwa yanayokingwa kwa chanjo imeendelea kuongezeka toka chanjo chanjo dhidi ya maradhi manne hadi tisa kufikia mwaka 2009 na kusema chanjo ya magonjwa ya kuhara na nimonia iliyozinduliwa inafanya maradhi yanayokingwa kwa chanjo kufikia 11.

"Magonjwa mengine yanayokingwa kupitia mpango wa Taifa wa chanjo ni kifua kikuu,ugonjwa wa Polio,Surua,kifaduro,Pepopunda,Dondakoo,Homa ya ini pamoja na Homa ya uti wa mgongo.

"Nachukua fursa hii kutoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Mara na Watanzania kwa ujumla wawwapeleke Watoto kwenye vituo vya kutolea Huduma ya chanjo ili kwakinga na maradhi haya na kubolesha maisha ya watu na uchumi wetu,"ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

Alisema pamoja na Serikali ya Tanzania kuhakikisha watoto wote walio na umri chini ya mwaka mmoja wanapata chanjo lazima ifahamike gharama ya chanjo hizo ni kubwa ambapo kila mtoa huduma,mzazi,mlezi viongozi pamoja na Wananchi wote kutambua gharama hizo.

"Gharama ya mtotot mmoja ni shilingi 51,218.85 kwa chanjo zote ambazo mtoto anazipata gharama ambazo hazijajumuisha kutoka kiwandani hadi kituo cha kutolea huduma ,gharama ya mabombaya sindano na mitungi ya gasi hivyo basi utaona Serikali ya Tanzania inavyotumia gharama kubwa kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa,"alisema.

Aidha Wazazi,Walezi pamoja na wanajamii wametakiwa kutambua kuwa jukumu la kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata chanjo kama haki stahiki ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika vituo vya kutolea huduma ya chanjo mbalimbali na huduma zingine ambazo zimekuwa zikitolewa kwa watoto.

Katika taarifa ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Dokta Samsoni Wenani ilisema idadi ya watoto waliopata chanjo imeongezeka kutoka asilimia 81 mwaka 2009 hadi asilimia 90 mwaka 2012.

Alisema chanjo pamoja na vifaa viligawiwa na kusambazwakatika Wilaya zote za Mkoa wa Mara Mwaka 2012 huku Mkoa ukiwa na lengo la kuchanja watoto chini ya Mwaka mmoja wapatao 91,062 katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2012 ambapo watoto walipatiwa chanjo mbalimbali.    

Post a Comment