-Aliyetekwa na kufanya kazi ya kupakia vichwa asimulia kila kitu
Mbunge Nyerere ataka askari walipwe
Na Shomari Binda
Musoma,
SUALA la
watu kutekwa na kukatwa vichwa limechukua sula nyingine baada ya mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Obwanga Jamara mkazi wa Utengi eneo la Ingili chini
katika Wilaya ya Rorya kutekwa na watu wasiofahamika na kuamuliwa kupaki vichwa
vya Binadamu katika visado vya rangi.
Akizungumzia
kisa cha kutekwa alipokuwa akizungumza na BLOG HII katika Hospitali
ya Mkoa wa Mara alikokuwa amelazwa katika chumba cha ICU kutokana na maumivu
makubwa aliyoyapata kutokana kwa watekaji alielezea kila kitu huku akilishitumu
Jehi la Polisi kwa kushindwa kufatilia.
Alisema
alifika katika Kijiji cha Nyankanga akitokea nyumbani kwake Utegi kwa lengo la
kukata mti wake wa mbao uliopo kijiji hapo Desema 27 na ndipo alipokutana na
dhahama ya kutekwa na kushuhudia maovu makubwa yanayofanywa na watekaji hao.
Alisimulia
kuwa alipokuwa katika maeneo hayo alikuwa katika maeneo hayo akiwa anatafuta
mashine ya kupasulia mbao ambapo huo ulikuwa mti wake wa pili kwenda kuukata na
mashine aliipata hapohapo kijijini kwa kukodi.
“Nilifika
Nyankanga nikiwa natafuta mashine baada ya mtu wa kwanza aliyenikodishia
kumkosa na kuanza kuulizia ndipo nilipokutana na vijana wawili ambao walidai
wanamfahamu mtu ambaye anayo mashine.
“Nilichukuliwa
na vijana hao na kufika mbele kidogo tulipanda kwenye gari inayodaiwa ndio
iliyokuwa ya mtu anayedaiwa kuwa na mashine ili kwenda kuufata nyumbani kwake
na kufika njiani niligeuziwa kibao.
“Nikiwa
nimewekwa katikati na wale vijana wawili nilitolewa mfano wa bastora nilipoiona
niligundua sio halisi pamoja na sime na kuambiwa nitoe pesa na mfuko wa ndani
nilikuwa na shilingi elfu sitini nikatoa na kuwapa,”alieleza.
Alisema
baada ya kutoa pesa hizo alifunikwa uso wake kwa shati lake alilokuwa amevaa na
kuwekwa nyuma ya buti ya gari na kupelekwa mahala kukojulikana ambako alikutana
na ukatili mkubwa unaofanywa na watekaji hao.
“Baada ya
kuzungushwa sana huku nikiwa nyuma ya buti ya gari niliingizwa ndani ya nyumba
ambayo siwezi kuifahamu na kuachwa humo na wenyewe kuondoka huku nikiwa bado
nimefungwa macho na kusikia sauti ya kike ikilia ndani ya nyumba hiyo.
“Baada ya
muda kupita watu wale walirejea na kunivua kitambaa machoni na kuniwekea box
mbele na kuniamulu nifungue na kukutana na vichwa vitatu vya Binadamu na
nilivyoviona ni vya watoto kati ya miaka mitatu ama mitano.
“Huwezi
kuamini ndugu Mwandishi ni hatari na Serikali isipo fatilia jambo hili hali
itakuwa mbaya sana maana suala hili lipo na mimi nimelifanya kwa mikono yangu
mwenyewe baada ya kutekwa.
“Nilivitoa
vile vichwa kwenye box nikishirikiana na Yule dada niliyemkuta mle ndani
nakuambiwa niviweke kwenye kisado cha rangi kimoja baada ya kimoja na kisha
kuweka udongo wa mfinyanzi huku jua tukiweka rangi na kufunga,”aliendelea
kusimulia muhanga huyo.
Alisema baada
ya kumaliza kufanya kazi hiyo aliyoamuliwa na watu waliomteka walimfunga tena
kitambaa machoni na kumtoa ndani ya nyumba na kumpakia nyuma ya buti ya gari na
kumpleka kusiko julikana.
“Tukiwa
njiani huku mimi nikiwa nyuma ya buti ya gari ilisimama na wale watu kushuka na
kuanza kuisukuma……inaonekana ilizimika lakini nilisikia watu wakipita
barabarani nakusalimiana habari afande July,”aliendelea kusimulia.
Alisema
baada ya gari kushindwa kuwaka na watu waliokuwa wakisalimiana nao kupita
aliwasikia watu hao wakipiga simu kuomba gari lingine na kuambiwa kuwa halipo
waangalie wafanyeje.
“Baada ya
gari kushindwa kuwaka walinishusha kwenye gari huku nikiwa bado nimefunikwa
macho na kupelekwa mahala na kutupwa huku mmoja wao akisema mmalizie kabisa
ambapo walinikanyaga kifuani na kichwani na kupoteza fahamu na kujua kuwa
tayari wameshaniua,”aliongeza.
KUOKOTWA NA POLISI MAKABURINI
Obwanga
alisema baada ya kupata nafuu katika chumba cha wagonjwa mahututi alisimuliwa
na wauguzi hospitali hapo kuwa alifikishwa na askari Polisi na kudaiwa
ameokotwa katika makaburi ya Menonite katika Manispaa ya Musoma Desemba 28.
Anadai baada
ya kufikishwa Hospitalini hapo hakuna askari yeyote aliyefika kwa muda
kumchukua maelezo ili wale waliofanya tukio hilo waweze kufatiliwa lakini
haikuwa hivyo.
“Hadi jana
(juzi) Desemba 30 saa mbili usiku ndipo nilipoona askari wanakuja kunichukua
maelezo nilitaka kugoma lakini nikaamua kutoa kutokana na kushauliwa na wauguzi
baada ya kuwaona Polisi hawatimizi majukumu yao kwa wakati,”alisema.
MEYA AZUNGUMZA NA KAMANDA
Baada
ya
kukutana na muhanga huyo kutokana na taarifa za Mwandishi wa Habari
hizi,Meya wa
Manispaa ya Musoma Alex Kisurura (Chadema) alikutana na Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma akiwa na muhanga na kukili
kupokea tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa kina.
"Tumeongea
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa na kutuhakikishia suala hilo linafanyiwa
kazi kwa nguvu zote na Jeshi na kuahidi kutoa matokeo yake baada ya
kukamilisha shughuli nzima,"alisema Meya Kisurura.
NYERERE ATAKA POLISI WALIPWE
Akizungumza kwa njia ya simu na Blog hii Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Vicenti Nyerere alisema kitendo cha askari Polisi kutokachukua hatua za haraka ni kutokana na baadhi yao kutolipwa mafao yao kwa wakati na kufanya kazi katika mazingira magumu.
Alisema zaidi ya askari 230 Mkoani Mara wanadai fedha zao hali inayopelekea kutokuwa na moyo wa kufanya kazi kwa ufanisi na kupelekea kutokea kwa matukio mbalimbali ambayo yanaweza kukabiliwa.
Post a Comment
0 comments