Musoma,
DIWANI wa kata ya Kigera
iliyopo katika Manispaa ya Musoma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Gabriel
Ocharo aliliomba Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kuandaa maandamano makubwa
yatakayokuwa na lengo la kuishinikiza Serikali kupeleka miradi ya Maendeleo
katika Manispaa hiyo.
Ocharo alitoa kauli hiyo
katika kikao cha Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo ambapo alidai Miradi mbalimbali
ya Maendeleo ambayo imekuwa ikipitishwa katika vikao vya bajeti imekuwa
haitekelezwi hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo kwa Wananchi.
Alisema Miradi hiyo ikiwemo
ya ujenzi wa zahanati,nyumba za walimu pamoja na miradi mingine inayotolewa
katika bajeti imekuwa haitekelezwi na Serikali na kuiacha Manispaa hiyo ikiwa
nyuma katika shughuli za kimaendeleo pamoja na elimu.
Diwani hayu alisema
haiwezekani kulikalia kimya suala hilo
huku Wananchi wakiendelea kwalalamikia madiwani kwamba hawafanyi kazi wakati
Serikali ya (CCM) inashindwa kutimiza wajibu wake wa kutekeleza miradi ambayo
imekuwa ikitolewa.
Nje ya kikao hicho Ocharo
aliliambia Gazeti la Mtanzania kuwa hapendi kuamini kama
Serikali inashindwa kupeleka miradi ya kimaendeleo katika Manispaa hiyo kwa
kuwa inaongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bali
anachokisema ni kwa nini miradi ya Maendeleo inashindwa kutekelezwa.
Alisema ipo miradi ambayo
ilitangazwa na Serikali katika Diwana wa kata ya Kigera iliyopo katika Manispaa
ya Musoma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Gabriel Ocharo aliliomba Baraza la madiwani
wa Manispaa hiyo kuandaa maandamano makubwa yatakayokuwa na lengo la
kuishinikiza Serikali kupeleka miradi ya Maendeleo katika Manispaa hiyo.
Ocharo alitoa kauli hiyo
katika kikao cha Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo ambapo alidai Miradi mbalimbali
ya Maendeleo ambayo imekuwa ikipitishwa katika vikao vya bajeti imekuwa
haitekelezwi hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo kwa Wananchi.
Alisema Miradi hiyo ikiwemo
ya ujenzi wa zahanati,nyumba za walimu pamoja na miradi mingine inayotolewa
katika bajeti imekuwa haitekelezwi na Serikali na kuiacha Manispaa hiyo ikiwa
nyuma katika shughuli za kimaendeleo pamoja na elimu.
Diwani hayu alisema
haiwezekani kulikalia kimya suala hilo
huku Wananchi wakiendelea kwalalamikia madiwani kwamba hawafanyi kazi wakati
Serikali ya (CCM) inashindwa kutimiza wajibu wake wa kutekeleza miradi ambayo
imekuwa ikitolewa.
Post a Comment
0 comments