0








Timu nzima ya inayoendesha kipindi cha Mini Buzz kinachorushwa kituo cha Televisheni cha TBC1 itakuwa Mjini Musoma na Tarime kwa kipindi cha wiki moja kuanzia jumatatu ya tarehe 18 mwezi wa 2 mwaka huu kwa ajili ya kufanya vipindi vyenye mada mbalimbali zinazohusu jamii.

Ukiwa ni mkazi wa maeneo hayo kuwa tayari kwa ajili ya kuchangia mada zitakazokuwa zikitolewa na kuwa na ushirikiano wa karibu ili kile kilichokusudiwa kiweze kuifikia jamii nzima ya Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.

Usiogope kutoa mchango wako mara Mini Buzz itakapokufikia katika eneo lako.

Post a Comment