MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara imetoa adhabu
ya kuchapwa viboko 24 kwa watu wawili
lucas Wancheka (17) na Saimoni Mnico(20) wakazi wa Bweri katika Manispaa ya Musoma waliokuwa wakituhumiwa kwa kosa la
kubaka mwanafunzi wa shule moja ya sekondari mjini hapa.
Akisoma Hukumu hiyo mbele ya mahakama,Hakimu Mkazi Mfawidhi Ramadhani Rugemalira
alisema kuwa watuhumiwa hao watachapwa viboko 12 kila mmoja baada ya Mahakama
kuridhika na maelezo ya mashahidi saba wa upande wa mashitaka.
Rugemarira
alisema shahidi wa kwanza ambaye ni mtendwa wa tukio hilo (Mwanafunzi) ambaye jina lake limehifadhiwa alidai
mbele ya Mahakama kuwa Machi 23 mwaka 2012 majira ya saa 1:00 usiku akiwa
anatoka shambani alikutana na vijana hao wawili aliowafahamu na kumshambulia
kwa kumpeleka vichakani kisha kumfanyia unyama wa kumbaka kwa zamu.
Maelezo ya Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa siku aliyofanyiwa unyama huo hakuweza
kutembea kutoka katika kicha alichokuwa amevutiwa bali alijitaidi kutambaa
hadi nyumbani kwa wazazi wake na kumuelezea mama yake mzazi yaliyomsibu.
Aliendelea
kusema kuwa baada ya kumweleza mama yake kuhusiana na kitendo alichofanyiwa
ndipo hapo mama mzazi alipochukuwa jukumu la kumpeleka mwanae kupata matibabu
hosptali.
Kwa upande
wake mwendesha mashitaka wa polisi Timoth Timoth aliiomba Mahakama kutoa adhabu
kali kwa watu hao waliotenda kosa hilo kutokana na kukithiri kwa matukio ya
ubakaji katika jamii.
Hata hivyo
hakimu Rugemarila alihukumu kesi hiyo kwa kuzingaia kifungu cha sheria namba 131A
(1 ),(2) na (3) kutokana na mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo kuwa na umri chini ya miaka
18.
Post a Comment
1 comments:
review buy tramadol next day - tramadol euphoria