0
Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Musoma,Denis Ekwabi alisema katika kikao kijacho cha Baraza la Madiwani wa Halimashauri hiyo atawaleta wataalamu wa vipimo kuhakikisha kila Diwani kabla ya kuingia katika kikao anapimwa virusi vya Ukimwi ili kuwa chachu kutoka kwa viongozi ili Wananchi wengine katika maeneo yao wapate kuelewa umuhimu wa kupima na kujua afya.

Ekwabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kupinga Ukimwi katika Halimashauri hiyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na blog hii kutokana na Kamati yake ilivyojipanga kuhakikisha watu wajitokeza na kupima kujua afya zao na kutoa uhasishaji kwa Wananchi kuepukana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Alisema Madiwani watakapoitikia kwa asilimia kubwa kupima kwa hiari kutawafanya Wananchi wengine kuona umuhimu wa suala hilo na kujitokea katika zahanati na vituo vya afya kujua afya zao na kupewa njia salama za kufuata baada ya kupima kutoka kwa wataalamu wa afya.

Alidai katika kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi katika Halimashauri hiyo kunapaswa kuwepo na ushirikiano wa karibu kutoka kwa viongozi,Wananchi na wataalamu wa afya ili mikakati iliyopangwa ya mapambano dhidi ya Ukimwi yaweze kutimia.

"Haya ni mapambano yetu wote ni muhimu madiwani wakiwa mfano wa kuigwa katika suala hili kwa kujitoa kupima kwa hiari naamini Wananchi nao wataitikia,Kamati yangu imejipanga kuhakikisha mipango yote iliyopangwa ya mapambano dhidi ya Ukimwi katika Halimashauri ya Wilaya ya Musoma inafanikiwa.

"Kikubwa Kamati haiwezi kufanya mapambano haya peke yake lazima tushirikiane kwa pamoja maana Jamii yetu itakapo athirika na Ugonjwa huu nguvu kazi ya Taifa itapotea na hata kazi za kijamii zitashindwa kufanyika na itakakuwa ndio chanzo cha kuendelea kuwa masikini,alisema Ekwabi.

Alisema jitihada zilizopo katika Halimashauri hiyo ni kuhakikisha unatoka katika nafasi ya nne kati ya wilaya sita zilizopo Mkoa wa Mara  ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi iliyopo kwa sasa kutokana na tafiti zilizofanywa ili kuendelea kuwa Wilaya salama ambayo haina maambukizi.

"Asilimia kubwa ya Madiwani wanayo taarifa ya zoezi hili la upimaji kwa hiari ambayo tuliitoa kupitia kamati ya kupinga Ukimwi katika Baraza lililopita,naamini katika baraza la Bajeti lijalo kila Diwani ataitikia na kupima kwa hiari na kutoa hamasa kwa Wananchi kufanya hivyo ili kuja afya na kuchukua hatua zinazofaa baada ya vipimo,aliongeza Ekwabi.

Akizungumzia hali ya maambukizi ya Ukimwi katika Halimashauri ya Wilaya ya Musoma,Mratibu wa Ukimwi wa Halimashauri hiyo Dk,Yusuph Kitunguye alisema kutokana na tafiti za mwisho zilizofanywa kwa mwaka 2007-2008 hali ya maambukizi katika Halimashauri hiyo ilikuwa 6.4 huku hatari zaidi ikionekana katika maeneo ya uvuvi na migodini.

Alisema katika matokeo ya upimaji yaliyofanywa katika kipindi cha januari hadi desemba mwaka 2012 hali ya maambukizi katika Halimashauri hiyo ilikuwa 4.1 na kusema jitihada za pamoja bado zinahitajika ili kupambana na maambuzi mapya ya virusi vya Ukimwi hasa sehemu hatarishi kama za mialo ,migodini na  sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi.

Dk,Kinguye alisema elimu mbalimbali bado inaendelea kutolewa kwa Wananchi kuhusiana na kujiepusha na ngono isiyo salama na kujiepusha na unywaji pombe kupindukia kwani kwa asilimia kubwa inachangia kufanya ngono bila kuchukua tahadhari na kupelekea kuingia kwenye hatari ya kupata virusi vya Ukimwi.  

Post a Comment