0
JESHI LA la Polisi mkoani Mara limewataka Wananchi kusherekea sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu bila kufanya matukio yoyote ambayo yatapelekea uharifu na uvunjifu wa amani kwa kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limejipanga kuhakikisha mtu ama watu watakaotumia kipindi hiki cha sikukuu kafanya uhalifu wanashughulikiwa.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Mara Absalom Mwakyoma alipokuwa akizungumza na BLOG HII namna ambavyo Jeshi hilo limejipanga kukabiliana na jambo lolote ambalo litataka kufanywa na mtu ama watu ambao wamekuwa wakitumia kipindi kama hiki kufanya uhalifu kwa kutumia mwanya wa watu wanapotoka katika majumba na kwenda kusherehekea katika maeneo mbalimbali.

Amesema yoyote ambaye atakuwa na mawazo ya kufanya vitendo vyovyote vya uhalifu aelewe kwamba ataishia mikononi mwa polisi kwa kuwa mipango madhubuti imepangwa kuhakikisha vitendo vyte vya kiuhalifu vinadhibitiwa kadri iwezekanavyo ili kila mmoja asherehekee sikukuu hii kwa amani.

Alida katika kipindi kama hiki cha sikukuu wapo watu ambao kazi yao ni kutumia mwanya wa sherehe kutaka kufanya uhalifuhivyo wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti vitendo vyote vya kiuhalifu na yoyote atakayekuwa na mawazo ya kufanya hivyo aache maana ataishia mikononi mwa polisi.

 Amesema licha ya Jeshi la polisi kujipanga vizuri kukabiliana na vitendo vya kiuhalifu kazi hiyo pia inapaswa kushirikiana na Wananchi kwa kutoa taarifa kutoka katika maeneo yao pale watakapoona hali yoyote ya wasiwasi kwa watu wasiowafahamu ili waweze kushughulikiwa kwa haraka.

Kamanda Mwakyoma amesema Wananchi ndio wanaokutana na wahalifu katika maeneo yao kwa asilimia kubwa hivyo popote watakapokuwa na taarifa juu ya uhalifu wasisite kutoa taarifa ili kuweza kukabiliana nao na kudhibiti uhalifu kabla haujatokea.

Kuhusiana na masuala ya ulevi,kamanda Mwakyoma amesema wale wanaotumia vyombo vya moto wajiepushe kuendesha wakiwa wamelewa kwani ajali nyingi zinatokea kutokana na ulevi pamoja na mwendo kasi na kipindi hiki cha sikukuu watu wanakuwa wengi barabarani hivyo ulevi na mwendo kasi hauhitajiki.

Aidha Kamanda Mwakyoma amewasisitiza Wananchi kutokuacha miji bila kuwa na watu ama watoto pekee yao kwani wahalifu wanaweza kuutumia mwanya huo kuingia ndani ya nyumba na kuchukua thamani za ndani.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Post a Comment