MADIWANI 16 wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamegomea kuingia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kushiriki kikao maalum cha Baraza la madiwani kwa ajili ya kumchagua makamu mwenyekiti kwa kile kilichoelezwa kupata maelekezo ya kugomea kutoka kwa viobgozi wa kitaifa wa Chama hicho.
Akitoa
maelezo kabla ya kufunguliwa kwa kikao hicho,Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo
Athman Akalama alisema amesikitishwa na kitendo cha madiwani hao kugomea kikao
hicho kwa kuwa walikuwa na taarifa ya wiki moja lakini ghafla walikigome mapema
kabla ya kuanza kwa kikao.
Alisema
kutokana na muongozo wa Tamisemi juu ya mabadiliko na uundwaji wa Halimashauri
mbili katika Wilaya hiyo ili lazimika kufanyika mchakato wa kuandaa muongozo wa
namna ya kuunda Halimashauri hizo na madiwani wa vyama vyote walishirikishwa
tangu hatua ya kwanza.
Akalama
alisema mabadiliko hayo kutoka Tamisemi kuingiza Mamlaka ya Mji katika
Halimashauri na kuundwa kwa Halimashauri mbili yan alengo la kuleta Maendeleo
kwa Wananchi wa Wilaya ya Tarime na hoja ambazo anadai zimetolewa na mwishoni
na madiwani wa Chadema ni kutaka kukwamisha Maendeleo.
Alisema hoja
ambazo zimetolewa na madiwani hao ni kutaka kupata orodha ya wajumbe wa
Halimashauri ya Mji wa Tarime pamoja na ukomo wa kamati zitakazoundwa baada ya
uchaguzi zikiwa katika maandishi hali ambayo hakuweza kuitekeleza kutokana na
kuitaka kwa uharaka.
Mkurugenzi
huyo wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime alisema madiwani hao hawakuleta maombi
ya hoja zao katika maandishi kama walivyoomba licha ya kuwa na muda wa kutosha na
walimpelekea barua ya uteuzi wa jina la mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti
tangu machi 18.
“Kwa kweli
mimi nashangaa uamuzi wa madiwani kutoka Chadema kugomea kikao hiki maana nimekaa
nao kwa muda wa kutosha na kupeana nao ushauri na maelekezo kuhusu jambo hili
lakini ghafla wamegomea,lakini kutoka na unyeti wa suala hili nawaomba
waheshimiwa madiwani mnipe muda wa kwenda kuwasikiliza tana ila kwa muda mfupi
ntaitisha Baraza tena,’’alisema Akalama.
Baada ya
Mkurugenzi kutoa maelezo hayo madiwa waliokuwa katika ukumbi huo kutoka CCM na
CUF walitaka kuendelea kwa kikao hicho na kufanyika kwa uchaguzi wa makamu mwenyekiti kwa kile
walichodai kuhailisha kikao hicho ni kufanya matumizi mabaya ya fedha za
Wananchi kwani ni ghalama kubwa kuandaa Baraza.
Kutokana na
hoja za madiwani wa vyama hivyo hatimaye uchaguzi wa kumpata makamu mwenyekiti
wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye ataongoza kamati mbili ambazo
ziliundwa kwa ajili ya ugawaji mali katika Halimashauri mbili za Wilaya ya
Tarime ulifanywa na madiwani 24 wakiwemo 23 kutoka CCM na 1 kutoka CUF ambapo
Diwani wa Kata ya Kitare Daud Wangwe (CCM) alishinda kwa kupata kura 23 dhidi
ya kura moja ya Diwani aliyekuwa amepitishwa na Chadema Charles Ndesi.
Akizungumza
na MTANZANIA,Diwani wa kata ya
Sababa Christopher Chomete (Chadema) ambaye alichaguliwa kuwa mmoja wa
wanakamati watakaohusika katika ugawaji wa mali alisema hautambui uchaguzi huo
kwa kuwa haukufuata utaratibu na hawezi kukubali kuwa katika kamati hiyo.
Alisema
taratibu
ambazo zimevunjwa ni pamoja na kutokuzingatia kanuni za kuendesha
baraza kwa kuwa theruthi mbili za wajumbe waliotakiwa kushiriki kikao
hicho hazikutimia bali waliendesha kikao hicho kwa kuitimia shinikizo la
madiwani wa CCM.
Chomete
alisema kutokana na kikao hicho kutokuwa halali hawezi kukubali nafasi
ya uteuzi wa mjumbe wa kamati kutoka Halimashauri ya Mji wa Tarime na
madiwani wote wanaotokana na Chadema hawataweza kuhudhuria vikao vyote
vilivyobaki vya Baraza la madiwani kama hawatabatilisha kikao
walichopfanya cha kumchagua makamu mwyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya
Tarime.
Post a Comment
0 comments