0


WALIOKUWA askari wa Jeshi la Polisi wa Biharamulo mkoani Kagera David Duma Dalema(36) na Gerald Tuji Kabalenga(33) pamoja na watu wengine wawili Boniphace John Kurwa(31) mkazi wa Geita pamoja na Mlangirwa Emanuel Paulo(32) (maarufu kama Mnyarwanda)wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mkoa wa Mara wakikabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la Uhujumu Uchumi. 

 Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mara Faisal Kahamba ilidaiwa na Wakili wa Serikali Kainunura washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama hiyo kutokana na kosa la Kuhujumu Uchumi na kuingia katika Hifadhi ya Taifa bila idhini kinyume cha kifungu namba 384 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shitaka lingine imedaiwa Mahakamani hapo mnamo januari 5 mwaka huu washitakiwa hao walikamatwa na nyara za Serikali kinyume cha kifungu 84 (1) ya sheria ya adhabu namba 5.

Aliiambia mahakama kuwa siku hiyo walipatikana na meno ya tembo
vipande 18 vyenye zito wa kilogramu 104 yenye thamani ya sh,69,750,000
mali ya serikali.
 

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa upya katika Mahakama hiyo kutokana na awali washitakiwa hao waliokamatwa na meno ya tembo vipande 18 vyenye uzito wa kilo 104
kufutiwa mashitaka na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kisha kukamatwa tena na kuhamishiwa Mahakama ya Mkoa wa Mara chini ya mwendesha mashitaka wa Serikali


Kuachiwa kwa watuhumiwa kisha kukamatwa kunatokana mwendesha mashitaka
wa Serikali kwa kushirikiana na Tanapa kuingilia kati baada ya
mwendesha wa mashitaka wa awali wa polisi Paskael
Nkenyenge kukaidi ushauri wa Hakimu wa Mahakama hiyo Amon Kahimba
kuwataka wabadilishe hati ya mashitaka .

Ushauri huo aliutoa machi 12 mwaka huu na kumtaka mpelelezi wa
kesi,mwendesha mashitaka na mkuu wa upelelezi mkoa wa Mara kubadili
mashitaka kwa madai kuwa yaliyopo ni dhaifu na mahakama inaweza
kuwaachia watuhumiwa hao wakati wowote.

Washitakiwa wote wanne wamerudishwa rumande hadi aprili 10 kesi hiyo itakapotajwa tena kutokana na kesi ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana
 

Post a Comment