0




UCHAGUZI wa wajumbe wa mabaraza ya Katiba ngazi ya mtaa uliofanyika siku ya jana katika mitaa 57 ya manispaa ya Musoma,huku ukigubikwa na vitendo vya kampeni za kisiasa na vurugu hali iliyopelekea baadhi ya wapambe wa wagombea kupigana ngumi huku mitaa mingine ikishindwa kufanya uchaguzi kutokanana vurugu hizo.

BLOG HII iliufatilia mchaguzi huo katika baadhi ya mitaa nakubaini baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wakiendesha kampeni za kuhimiza kuchaguliwa kwa wagombea wanaotokana na vyama vyao katika kuwapata wajumbe wanne wa baraza kutoka katika makundi ya wazee, wazazi,.wanawake na vijana.

Usiku wa kuamkia uchaguzi baadhi ya wafuasi wa vyama vya kisiasatu walipita katika majumba wakiomba kura ili wawe wajumbe katika mitaa na kuibuka kwa maswali kutoka kwa Wananchi nini kikubwa ambacho watu hao wanachotaka kwenda kufanya katika baraza la katiba la Wilaya.
Mwandishi wa habari hii alishuhudia wafuasi wa mgombea mmoja aliyeshindwa kwa nafasi ya wazazi katika mtaa wa Mwigobero "B"wakichapana makonde na wafuasi wa mmoja wa  wagombea aliyeshinda katika nafasi hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuletwa kwa wapiga kura mamluki wasio wakazi wa mtaa huo.

Afisa Mtendaji wa kata ya Mwigobero Mathias Makunja alikili kutokea kwa vurugu katika mtaa huo kutokana na ushabiki wa kisiasa lakini baadae zilitulia na kuendeshwa kwa uchaguzi na mitaa yote minne ilimaliza salama uchaguzi na kuwapata wajumbe wanne kutoka kila mtaa.

Katika mtaa wa Mtakuja uliopo kata ya Mwisenge,uchaguzi huo ulihailishwa kutokana na kuzuka kwa vurugu baada ya Wananchi kudai usiku ulikuwa umeingia kutokana na kucheleweshwa kwa zoezi la upigaji kura na kudai kuwa wasingeweza kupiga kura katika kuwachagua wajumbe wa makundi yote manne.

Kwa mujibu wa taarifa ya msimamizi wa uchaguzi katika mtaa huo,Samson Nakuzerwa ambaye ni Mtendaji wa mtaa alisema Wananchi walichelewa kuja katika mkutano wa uchaguzi ingawa muda ulikuwa bado unaruhusu lakini Wananchi walichelea giza kuathiri shughuli zote za uchaguzi hivyo kulazimika kuhailishwa zoezi zima.

Aidha kwingineko katika mtaa wa Nyasho "C" kulizuka vurugu kubwa baada ya uchaguzi kufuatia baadhi ya vijana kukerwa na kampeni za wazi za kisiasa zilizoendeshwa katika uchaguzi huo na wafuasi wa mgombea mmoja wa kundi la wazazi hali iliyopelekea kuitwa kwa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia na kuwatawanya vijana hao.

Mratibu wa zoezi hilo kutoka Halimashauri ya Manispaa ya Musoma Msiranga Msiranga alisema taarifa alizonazo ni kutokufanyika kwa uchaguzi katika mtaa wa Mtakuja lakini taarifa kutoka katika mitaa mingine bado hajazipata na pale atakapozipata atatoa taarifa ya zoezi zima.


Post a Comment