SERIKALI,BENKI YA MAENDELEO AFRIKA(ADB) YAKAMILISHA JENGO LA MAABARA MUSOMA
SERIKALI nchini kwa kushirikiana na benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imegharamia kiasi cha dola laki 6 za kimarekani katika ujenzi wa maabara ya kisasa katika hosptali ya mkoa wa Mara.
Taarifa hiyo ilitolewa na kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Martin Khan wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari hosptalini hapo.
Alisema hosptali hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na maabara yenye hadhi ya kimkoa kwa kile alichosema iliyokuwepo ilikuwa ndogo na pia vifaa vilikuwa vichache ambavyo avikidhi mahitaji.
Khan alidai kulikuwa na hitaji kubwa la vifaa vya mahabara katika hospitali hiyo kutokana na asilimi kubwa ya wagonjwa kutoka katika Wilaya zote za mkoa huo kutegemea huduma kutoka hapo hivyo msaada huo umekuja katika wakati muwafaka katika kukabiliana na uhaba huo
“Wagonjwa walikuwa wanashindwa kupata majibu kwa muda muafaka kwa sababu jengo la maabara lilikuwa dogo hivyo wataalamu wa maabara walikuwa katika vyumba tofauti hivyo ni lazima mgonjwa ahame kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili aweze kupata majibu yake yote kwa pamoja”alisema Dkt Khan.
Khan alisema kuwa kukamilika kwa maabara hiyo ni chachu kubwa sana kwa wagonjwa hapa mkoani kwa sababu alizoelezea kuwa maabara hiyo hutumiwa na wagonjwa wa mkoa mzima ila kwa wale wanaoelekezwa na waganga wa wilaya wanazotoka.
Nae Kaimu Mkuu wa maabara hiyo Dkt Zephania Nzungu alielezea kukamilika kwa maabara hiyo kumesaidia hosptali hiyo kuwa na sifa nzuri kwa wananchi tofauti na hapo awali.
“Wananchi wa hapa mkoani walikuwa wakidharau sana maabara ya hapa hosptalini,huku wengi wao wakitumia maabara za mitaani na za hosptali binafsi, lakini baada ya kukamilika kwa hii maabara wagonjwa wenyewe wamekuwa na imani na vipimo vya majibu ya magonjwa yao”alisema Nzungu.
Kulikuwepo na changamoto nyingi za huduma za afya mkoani hapa ambazo zilikuwa zinachangiawa kutokuwepo kwa maabara ya kisasa,hivyo kupatikana kwa maabara hiyo iliyoanza kujengwa Machi 2010 na kukamilika Desemba 2010 imesaidia kuboresha huduma za maabara mkoani hapa.
Post a Comment
0 comments