0




MBUNGE wa viti maalum kupitia vijana mkoani Mara Ester Bulaya (CCM) ameipongeza timu ya soka ya maafande wa polisi Bunda baada ya kuibuka mabingwa wapya katika ligi ya mkoa wa Mara ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi dhdi ya timu ya Musoma shooting unaofanyika hii leo ijumaa mjini Bunda.

Akizungumza na BLOG HII kwa njia ya simu baada ya kupata taarifa za kuchukua ubingwa kwa timu hiyo,Bulaya alisema timu hiyo imeonyesha njia nyingine ya mabadiliko katika soka la Wilayani Bunda na mkoa wa Mara kwa ujumla kwa kuwa ni muda mrefu wilaya ya Bunda haijawahi kutoa bingwa wa mkoa.

Alisema timu hiyo imechukua ubingwa kutokana na maandalizi iliyokuwa nayo ya muda mrefu na ushirikiano wa karibu uliokuwepo baina ya viongozi wa timu hiyo pamoja na wadau wengine wa soka ambao ushirikiano uliokuwepo ndio mafanikio ya timu hiyo kuchukua ubingwa wa mkoa wa Mara msimu huu.

Bulaya alisema hatua iliyofikia timu hiyo inastahili kupongezwa kutokana na ushindani uliokuwepo katika ligi ya msimu huu kutoka kwa timu ngumu ambazo zimeshiriki ligi ya mkoa huo kwa muda mrefu kama Kigera fc ya Manispaa ya Musoma,Polisi Tarime pamoja na Musoma Shooting ambazo zimekuwa na uzoefu wa muda mrefu katika mashindano.

"Niipongeze sana timu ya Polisi Bunda baada ya kuchukua ubingwa wa mkoa wa Mara msimu huu,najua ligi ilikuwa ngumu na wachezaji wamejituma uwanjani pamoja na ushirikiano wa benchi la ufundi na hatimaye lengo limefanikiwa hivyo hakuna budi kutoa pongezi nyingi sana kwa wote waliofanikisha ubingwa ukapatikana,"alisema Bulaya.

Mbunge huyo alidai kuwa safari bado ni ndefu kwa timu hiyo baada ya kuchukua ubingwa wa mkoa hivyo ushirikiano wa karibu unahitajika baina ya wadau wote wa soka katika Wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara kwa ujumla ili iweze kufanya vizuri tena katika ligi ya Taifa na hatimaye kuingia ligi daraja la kwanza na kuanza jitihada za kuhakikisha tunapata timu ya ligi kuu.

Ubingwa wa timu ya Polisi Bunda umekuja baada ya kuingia hatua ya nne bora katika ligi ya mkoa hu iliyoshirikisha timu 10 kwa kuzifunga timu za Polisi Tarime na Bunda Town Stars na kufikisha pointi 6 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ambazo zilifanya vibaya katika michezo yao mingine.

Wadau wa soka mjni Bunda wameeleza kuwa kuchukua ubingwa kwa timu hiyo ni kutokana na jitihada za Mbunge huyo kuhamasisha michjezo katika Wilaya hiyo kupitia mashindano ya Ester Bulaya Cup ambayo hufanyika katika Wilaya hiyo kila mwaka na kuibua vipaji vingi vya soka.

Post a Comment