KIKOSI cha timu ya
soka ya Waandishi wa Habari mkoani Mara Habari fc kimeanza mazoezi kwa ajili ya
bonanza la Waandishi litakalofanyika siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (Media
Day) mey 3 katika viwanja vya posta Mjini Musoma.
Akizungumzia bonanza
hilo,Mratibu wa bonanza George Marato alisema tayari maandalizi yanaendelea
vizuri katika kufanikisha bonanza hilo ambalo litawashirikisha wadau mbalimbali
wa Habari kwa lengo la kufahamiana na kujenga mahusiano.
Alisema mazoezi wameamua
yaanze mapema katika mchezo wa mpira wa miguu ili kuandaa kikosi ambacho
kitaendeleza rekodi ya kutokufungwa na timu yoyote tangu ilipoanzishwa na
kutamba kuendelea na wimbi la kushinda katika michezo ambayo wanakutana na kila
timu wanayokutana nayo.
Marato alisema bado
wana kikosi kizuri cha timu ya mpira wa miguu licha ya kuwakosa kikosini
wachezaji wao wawili Mabere Makubi na Cales Katemana ambao wameamia katika
mikoa mingine ya vituo vipya vya kazi lakini wanaamini kuendeleza rekodi hiyo
ya ushindi katika bonanza hilo.
"Katika bonanza
hilli licha ya mchezo wa soka tutakuwa na michezo mingine kama riadha,kuvuta
kamba,kukimbia kwenye magunia pamoja na kufukuza kuku yote haya tunayafanyia
maandalizi na tunawashirikisha wadau mbalimbali katika kufanikisha siku hii
ambayo itawakutanisha Waandishi wote wa mkoa wa Mara pamoja.
"Kwenye mpira wa
miguu tumepanga kucheza na timu ya wakusanya kodi wa TRA Mara maana tuliwafunga
na kuchukua kombe walioandaa wenyewe katika siku ya mlipa kodi sasa tunataka
tuwadhihilishie kuwa hatukubahatisha pale tulipowafunga kwenye mchezo
huo,"alisema Marato.
Mratibu huyo wa
bonanza la Waandishi wa Habari alisema kabla ya kufanyika kwa bonanza hilo
watakutana na wadau wa soka pamoja na michezo mbalimbali ili kuona namna ya
kusaidiana na kurudisha hamasa ya michezo katika Manispaa ya Musoma pamoja na
mkoa wa Mara kwa ujumla.
Alidai hamasa ya
michezo imepungua tofauti na zamani na kwa sasa michezo imekuwa ikifanyika
kwenye ligi za soka na inapomalizika wachezaji wanakaa mwaka mzima bila kufanya
michezzo hivyo kuendelea kudumaza michezo ambayo kwa sasa imekuwa ni sehemu ya
ajira na kujiongezea kipato.
Post a Comment
0 comments