MBUNGE wa jimbo la
Musoma Mjini Vicent Nyerere (CHADEMA) ametoa msaada wa mifuko mitano ya saruji
kwa ajili ya kufanyia ukarabati choo cha msikiti wa Rahman Nyakato katika
Maniuspaa ya Musoma ambacho kimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Mkoani Mara.
Akikabidhi msaada huo
kwa niaba ya Mbunge,Katibu wa Mbunge Fikiri Malenge alisema viongozi wa msikiti
huo walifika katika ofisi ya Mbunge na kuomba msaada huo kutokana na kuharibiwa
kwa choo hicho baada ya mvua ambazo zilifululiza katika kipindi cha hivi
karibuni.
Alisema kutokana na
umuhimu wa suala hilo Mbunge aliamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuanza
kukarabati choo hicho ili waumini waendelee kufanya ibada bila kuwa na kikwazo
pale inapoihitajika huduma ya choo.
"Kama
tunavyofahamu Mbunge kwa sasa yupo kwenye vikao vya Bunge la Bajeti kule Dodoma
lakini baada ya kupata taarifa hizi ameanza na msaada wa mifuko hii ya saruji
lakini ameahidi kuendelea kusaidia ili ukarabati huu uweze kukamilika haraka na
atakapotoa maelekezo mengine tutawasiliana na viongozi wa Msikiti,"alisema
Fikiri.
Katibu huyo wa Mbunge
alisema Uongozi wa Msikiti wa Rahman katika kukamilisha ukarabati wa choo hicho
licha ya kuhitaji saruji pia kunahitajika vifaa mbalimbali vya ujenzi ili
kuweza kukamilisha choo hicho ambapo Mbunge Nyerere ameahidi kuwa na
mawasiliano na uongozi wa msikiti ili kukamilisha suala hilo.
Akipokea mifuko hiyo
ya saruji,Katibu wa Msikiti huo Ustadh Iddy Ndimila alimshukuru Mbunge Nyerere
kwa kuwa mtu wa kwanza kuona umuhimu wa suala hilo na kuchangia katika kuanza
kukarabati choo hicho kilichoaribiwa na mvua.
Alisema Nyerere
ameonyesha njia ya kusaidia kukamilisha suala hili lakini bado kuna mahitaji
zaidi yanayohitajika hivyo kumuomba kila mmoja kuweza kuguswa na jambo hilo na
kufika katika msikiti huo na kusaidia sehemu ya mahitaji yanayohitajika.
"Bado
tunauhitaji wa mchanga,tofari,mbao na vifaa vingine vya ujenzi yoyote anaweza
kusaidia na kila atakayetoa katika hili malipo yake tunayakabidhi kwa mola na
msaada wake anaweza kuuleta pale msikitini Nyakato ama akapeleka katika msikiti
mkuu wa Ijumaa na utatufikia,"alisema Ustadh Iddy.
Post a Comment
0 comments