Taasisi ya kifedha isiyokuwa ya
kiserikali inayojishughulisha na mikopo Finca Tanzania Tawi la Musoma imesema
kutokana na tatizo la ajira hapa Nchini Watanzania wanayo nafasi ya kukopa na
kufanya ujasiliamali ambao utawaongezea kipato na kuendesha maisha ya kila
siku.
Akizungumza na BLOG HII
ofisini kwake,Meneja Wa Finca tawi la Musoma Patrick Swenya alisema bado kuna
nafasi ya kujiajili kwa mtu yeyote kupitia ujasiliamali kwa kuchukua mikopo
katika taasisi za kifedha na kuendesha biashara mbalimbali.
Alisema Finca kwa sasa imeongeza wigo
wa huduma zake hapa Nchini kupitia matawi mbalimbali ambayo yanawawezesha
Wananchi kuchukua mikopo na kuendesha biashara ambazo zinaweza kupunguza kasi ya
ukali wa maisha.
Swenya alisema Finca ili kuhakikisha
Wananchi wanaochukua mikopo katika taasisi hiyo wananufaika nayo ina utaratibu
wa kuendesha mafunzo ya ujasiliamali na biashara kutoka kwa maofisa wake kwa
wahitaji wa mkopo kabla ya kuwapa mikopo hiyo.
Alisema kutokana na tatizo la ajira
kwa sasa hapa Nchini,amewaomba Vijana
wanaotoka vyuoni kuacha kutegemea ajira za Serikalini bali wanaweza kuendesha
maisha kwa kujiajili kwa kufanya biashara kutokana na kuchukua mikopo katika
taasisi za fedha.
"Vijana
wengi wanaohitimu masomo vyuoni kila mmoja anataka aajiliwe Serikalini
hili haliwezekani maana tunashuhudia ajira zilivyo chache hapa Nchini
hivyo hakuna budi kuwa wajasiliamali kwa kutafuta fedha katika taasisi
za fedha ili wajikomboe,"alisema Swenya.
Alidai Finca bado inayo nafasi kwa
mtu yoyote anayehitaji kujiajili kwa kuchukua mkopo na kufanya biashara
kujiunga katika vikundi ama mtu binafsi milango bado ipo wazi katka taasisi
hiyo hivyo fursa itumiwe katika
kujiletea Maendeleo.
Akizungumzia uanzishwaji wa huduma za
kibenki katika taasisi hiyo Makao Makuu Jijini Dar es salaam,Meneja wa Finca
tawi la Musoma alisema huduma hiyo kwa sasa inatolewa katika matawi yake matatu
Jijini humo na utaratibu unaendelea kufanyika ili huduma hizo za kibenki ziweze
kufanyika katika matawi mengine.
Post a Comment
0 comments