JESHI
la polisi mkoani Mara limekamata bunduki nne zinazodaiwa kutumika
katika matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yamekuwa yakilipotiwa
kutokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kupelekea watu kudhuliwa
na kunyang'anywa mali.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari
juu ya utekelezaji wa oparesheni iliyoendeshwa katika kipindi cha miezi
mitatu,kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema kukamatwa
kwa bunduki hizo kunatokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa
Wananchi wema.
Alisema katika kipindi cha kuanzia mwezi januari
hadi machi,jeshi la polisi limekuwa likiendesha oparesheni za mara kwa
mara na kufanikiwa kukamata bunduki hizo shortgun moja,SMG moja pamoja
na magobore mawili pamoja na risasi nne zilizokuwa
zikitumiwa katika matukio ya uhalifu.
Kamanda Mwakyoma alisema
kutokana na oparesheni hiyo ambayo alidai itakuwa ni endelevu pia
walifanikiwa kukamata siraha za jadi kama mishale,marungu,mapanga na
nondo pamoja na watuhumiwa hamsini na sita (56) ambao walifikishwa
mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Alisema katika
oparesheni hiyo ambayo iliendana na misako mbalimbali katika Wilaya za
Serengeti,Bunda,Musoma pamoja na Butiama walifanikiwa kukamata makosa
mbalimbali na vielelezo ikiwa ni pamoja na kusambaratisha vikundi vya
uhalifu vilivyokuwa vimejitokeza kwa kipindi hicho.
"Katika
kipindi cha kuanzia mwezi januari mwaka huu viliibuka vikundi vitano (5)
vya uhalifu katika Manispaa ya Musoma ambavyo ni Makirikiri,Jamaica
mokas,Mbio za vijiti,Mdomo wqa furu pamoja na West lawama ambavyo vyote
tumefanikiwa kuviosambaratisha na tutaendelea kuhakikisha hakuna kikundi
chochote cha uhalifu kinakuwepo.
"Vikundi hivi
kwa sasa vimetoweka baada ya kufanikiwa kusambaratishwa kwa kuwakamata
viongozi wapatao 10 wa vikundi na kuwafikisha Mahakamani ambapo mpaka
sasa kesi zaio zinaendelea na kiasi furani hali ya amani ipo baada ya
vikundi hivyo kusambaratishwa,"alisema Mwakyoma.
Kamanda Mwakyoma
alisema katika kipindi hicho cha miezi mitatu jeshi la polisi
lilifanikiwa kukamata watuhumiwa 62 wa madawa ya kulevya ya bangi na
mirungi ikiwa ni pamoja na bangi kilo 69.6 na mirungi kilo 34.
Aliongezea
kuwa katika kupambana na vitendo vya uharamia,jeshi la polisi
lilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 68 pamoja na vipande 26 vya
pembe za ndovu ambapo watuhumiwa watano walifiokishwa mahakamani
kutokana kukutwa na nyara hizo za Serekali.
Home
»
»Unlabelled
» BUNDUKI NNE ZA UHALIFU ZAKAMATWA MKOANI MARA
Post a Comment
0 comments