0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya mkoa wa Mara imemuhukumu kifungo cha miaka 56 jela mkazi wa Songea mkoni Ruvuma Jossey Joseph (36) baada ya kupatikana na hatia ya makosa 8 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa waumini wa makanisa ya Anglicana na Nyumba ya Mungu yaliyopo katika Manispaa ya Musoma.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa Serikali Theophil Nestory mnamo mwezi wa 7 mwaka 2002 mtu huyo alifika katika makanisa hayo na kudai ana Shirika lisilo la kiserikali (NG'o) liitwalo FRUCULT OF LIVING POWER ambayo inajihusisha kusaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatafutia kazi,vyuo pamoja na bima za afya kinyume cha kifungu cha 301 na 302 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Ilidaiwa mtu huyo alidai kiasi cha shilingi elfu ishilini na elfu kumi na tano kutoka kwa watumishi 80 kwa ajili ya kuendesha semina katika shule ya msingi Azimio iliyopo katika Manispaa ya Musoma kwa ajili ya maandalizi ya kupatiwa kazi.

Alidai licha ya kuahidi kuwatafutia ajira walio katika mazingira magumu pia aliwaeleza waumini hao kuwa ana njia rahisi ya kuwaunganisha katika bima ya afya ambayo itawawezesha kupata matibabu bila usumbufu pale watakapokuwa na maradhi.

Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kuieleza Mahakama kuwa katika kufanya ufatiliaji juu ya taasisi hiyo iligundulika ilikuwa ni utapeli kwa kuwa hakuna taasisi kama hiyo iliyofanyiwa usajili ambayo inafanya kazi za kusaidia walio katika mazingira magumu kwa kuwatafutia kazi.

Kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya utapeli na kuibuka kwa taasisi ambazo hazina malengo ya kuwasaidia Wananchi,mwendesha mashitaka huyo aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

Akisoma Hukumu ya kesi hiyo,Hakimu wa Mahakama hiyo Emanuel Ngigwana alidai baada ya kusikiliza upande wa mashitaka katika kei hiyo bila kuwa na shaka yoyote alitoa huku ya miaka 56 sawa na miaka 7 katika makosa 8 huku adhabu zote zikienda kwa pamoja ili kuwa fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na makosa ya utapeli.

Post a Comment