0

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) mkoani Mara imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Halimashauri ya wilaya ya Musoma pamoja na Halimashauri ya Manispaa ya Musoma kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka.

Watumishi  kutoka katika Halimashauri ya Wilaya ya Musoma Iscary Silla Mlassa ambaye ni Afisa Ugavi Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi (PMU) na Eliuter Mhavile Nywage aliyekuwa kaimu Mkurugenzi kuanzia tarehe 5/8/2011 hadi 16/8/2011 walifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka ya  mbele ya hakimu mkazi Emmanuel Ngigwana na mwendesha mashitaka wa Takukuru Erick Kiwia.

 Mwendesha mashitaka wa Takukuru Kiwia alisema watumishi hao walifanya kosa la matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Akifafanua makosa hayo Kiwia alisema kuwa watumishi hao kwa pamoja walifanya uteuzi wa wajumbe wa timu ya tathimini ya zabuni  namba LGA/066/2011-2012/N/01,ambao waliandaa taarifa ya tathimini ya zabuni  na kuipendekeza kampuni ya M/S Vitrece Oil Mills(2004) T.LTD baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyohitajika.

Alisema mshitakiwa wa kwanza baada ya kupokea taarifa hiyo ya tathimini hakuiwasilisha katika kikao chochote cha bodi ya zabuni ya halimashauri hiyo ili ikubaliwe au ikataliwe bali alishirikiana na mshitakiwa wa pili na kuteua timu nyingine mpya ya tathimini kwa ajili ya kufanya tathimini ya zabuni hiyo tena pasipo kutoa sababu za kufanya hivyo.

Hakimu Gigwana alisema  kesi hiyo itatajwa tena Juni 06 mwaka huu na kwamba washitakiwa wana haki ya kupata dhamana baada ya kutimiza mashariti ya zamana.

Akisoma mashariti ya dhama alisema kila mmoja atatakiwa kuweka dhamana ya sh 3 milioni,wadhamini wawili wanaotambulika na mmoja kati ya hao wawili awe mtumishi wa serikali.

Katika kesi nyingine ya Takukuru iliyofikishwa katika Mahakama hiyo ilimuhusu aliyekuwa Kaimu Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Musoma Arnold Zephania kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka kinyume cha kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Mbele ya Hakimu wa Makama hiyo Janeth Msarocha,ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa Takukuru  Mwema Mella mnamo januari 6 mwaka 2012 alishiriki katika kikao akiwa mjumbe wa kamati ya ugawaji wa aridhi iliyokaa kwa kwa ajili ya kugawa viwanja vilivyoko eneo la Bweri katika Mabnispaa ya Musoma.

Ilidaiwa katika kikao hicho mtuhumiwa huyo akiwa katibu wa kikao hicho aliandika jina lake pamoja na majina ya watumishi wengine wa Halimashauri hiyo ili waweze kugawiwa viwanja katika maeneo hayo.

Mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru aliieleza Mahakama kuwa uchunguzi ulithibitisha mshitakiwa hakuingiza majina ya wakazi wa awali wa maeneo hayo waliokuwa wakiyamiliki maeneo husika.

Post a Comment