2



MAANDALIZI ya kumtafuta mrembo atakeuwakilisha mkoa wa Mara katika mashindano ya urembo ya ngazi ya Kanda na baadae Taifa yameanza kufanyika ambapo jumla ya warembo 18 kutoka katika Wilaya za Mkoa huo wanatarajiwa kuingia kambini kesho   kwa ajili ya kinyang'anyiro cha Redds miss Mara 2013.

Akizungumza na Mtanzania,muuandaji wa shindano hilo Goldon Mkama kutoka kampuni ya Homeland Entertainment alisema maandalizi ya kambi hiyo ambayo itakuwa katika hotel Maltivila yameshakamilika na tayari warembo wote wanaotarijiwa kushiriki shindano hilo wameshapewa taarifa.

Alisema katika shindano la mwaka huu kuna tegemewa kuwa na ushindani mkubwa baada ya warembo wengi kuchukua fomu kwa ajili ya ushiriki wa shindano hilo baada ya kupata nafasi za juu katikaka mashindano ya urembo ya Wilaya ambayo yamemalizika hivi karibuni.

Mkama alisema katika shindano la kumsaka mrembo wa miss Tarime kulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa washiriki walioshiriki shindano hilo hivyo kulazimika kuchukua washiriki watano ili waweze kushiriki shindano la mkoa.

"Muitikio umekuwa mkubwa katika shindano la mwaka huu maana warembo wengi wamejiamini na kujitokeza kushiriki mara baada ya kupata taarifa juu ya shindano hili hivyo ni matarajio yangu Redds miss Mara mwaka 20013 litakuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo.

"Serengeti pia kulikuwa na ushindani mkubwa katika kinyang'anyoro cha shindano la  Wilaya ambapo tumechukua washindi wa kwanza hadi wa tatu ambao wataingia kambini kwa ajili ya kushiriki shindano la mkoa ambalo litafanyika juni 7 Manispaa ya Musoma,"alisema Mkama.

Muandaaji huyo wa shindano la Redds miss Mara 2013 alidai warembo watakaoingia kambini watakuwa chini usimamizi wa miss Talent 2012 katika shindano la miss Tanzania Babylove Kalala ambapo amewataka warembo wote kuzingatia nidhamu ya kambi katika kipindi chote cha kambi.

"Hatutasita kumuondoa kambini mrembo yoyote ambaye atakwenda kinyume na utaratibu wa kambi kwa mujibu wa masharti hivyo lazima utaratibu ufuatwe na kuzingatia yale ambayo yamejazwa katika fomu a ushiriki wa shindano,"aliongeza Mkama.

Post a Comment

Νο matteг if some one searches for hiѕ
essеntial thing, thus he/she wіshes to be available
that in dеtail, thus that thing is maintained οvеr here.


mу blog :: Lloyd Irvin

Eѵerything іs ѵery open ωіth a verу сlеаr сlarifіcаtіon of the сhallengeѕ.
Ιt wаѕ definitely informatiѵe.
Your website is useful. Тhanks foг sharing!


Also visіt my wеb sitе :: reputation management