TAASISI ya Kuzui na
Kupambana na Rushwa mkoani Mara (TAKUKURU) imemfungulia Shauri la jinai namba
85 ya mwaka 2013 inayohusu matumizi mabaya ya mamlaka aliyekuwa Katibu Twala wa
mkoa wa Mara Clement Lujaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoni humo.
Mashitaka hayo ya
matumizi mabaya ya mamlaka yamefikishwa Mahakamani mbele ya Hakimu Janety
Musalocha na Mwendesha mashitaka wa Takukuru Elick Kiwia.
Akitoa ufafanuzi wa
mashitaka hayo,Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara Holle Makungu amewaeleza Waandishi
wa Habari kati ya tarehe 15 februari 2010 na julai 2011 Katibu Tawala huyo kwa
kutumia wadhifa wake kama Afisa Masuhuri wa mkoa wa Mara kwa nyakati tofauti
katika kipindi hicho alidhiinisha magari ya Serikali yaliyo chini ya usimamizi
wake yafanyiwe matengenezo katika karakana (garage) za watu binafsi pasipo
kukaguliwa.
Alisema kutokana na
utaratibu uliopo,magari yote ya Serikali yanatakiwa kupata kibali cha
matengenezo kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) hivyo kitendo cha
Katibu Tawala huyo kupeleka katika karakana za watu binafsi ni kinyume cha
utaratibu.
Mkuu huyo wa Takukuru
alieleza kuwa kutokana na kitendo hicho kulipelekea watu binafsi kujipatia
faida bila ya uhalali jumla ya kiasi cha shilingi milioni kumi na nane,laki
nane, therathini na sita elfu,mia nane na tano (18,836805/= kitendo ambacho ni
matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya kuzuia na
Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kesi hiyo ambayo
imefunguliwa bila ya mshitakiwa kuwepo Mahakamani kwa kuwa hayupo Mjini Musoma
imepangwa kutajwa tena Mahakamani hapo juni 18 ambapo mshitakiwa ametakiwa
kuwepo siku hiyo ili aweze kujibu shitaka linalo mkabili.
Hakimu Musaroche
ametoa hati ya wito kwa mshatakiwa chini ya kifungu cha 100 cha Sheria ya
Mwenendo wa Mkosa ya Jinai,Sheria namba 20 kama ilivyofanyiwa Mapitio mwaka
2002 inayomtaka mshitakiwa kufika katika Mahakama hiyo tarehe tarehe 18/6/2013.
Takukuru mkoa wa Mara
imewataka maafisa masuhuri katika Mamlaka za Umma ikiwa ni pamoja na makatibu
Tawala wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halimashauri,Wakala wa Serikali ambao wana
mtindo wa kutengeneza magari ya Umma katika karakana za watu binafsi bila
kufuata utaratibu sahihi wa kisheria wa matengenezo ya magari ya Serikali
kuacha kufanya hivyo.
Mkuu huyo wa Takukuru
mkoa wa Mara alisema ofisi yake italazimika kuanzisha uchunguzi dhidi ya
maafisa masuhuri ambao wanafanya vitendo hivyo ili sheria iweze kufuata mkondo
wake.
Kufikishwa kwa
aliyekuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mara na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa kunafikisha idadi ya watumishi wa nne kufikishwa Mahakamani na Taasisi
hiyo katika kipindi cha wiki moja ambapo awali walifikishwa watumishi wawili
kutoka Halimashauri ya Wilaya ya Musoma na mmoja kutoka Halimashauri ya
Manispaa ya Musoma kutokana na matumizi mabaya ya Mamlaka.
Post a Comment
0 comments