0


WATU wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mara kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kamnyonge iliyopo katika Manispaa ya Musoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kituo kikuu cha pilisi kati mjini hapa, kamanda wa jeshi hilo Absalom Mwakyoma alisema watu hao aliowataja kwa majina ya Juma Hassan (34) na Makundi Mwita wote wakazi wa Nyakato wakihojiwa kutokana na tukio hilo lililotokea mei 28.

Kamanda Mwakyoma alimtaja mwanafunzi  aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu cha ncha kali kali katika shavu la kulia pamoja na paja la kulia kuwa ni Ester Elias (15) ambaye aliondoka nyumbani kwao Mei 27  siku ya Jumatatu  asubuhi kuelekea shule na aliporudi aliaga kuwa anafatilia madaftari pamoja na tai yake na hakuweza kurudi hadi alipokutwa akiwa amefariki karibu na nyumbani kwao.

 “Ndugu wa binti huyo walipoona haonekani kurudi nyumbani walianza kumtafuta na kutoa taarifa kituo cha polisi,hata hivyo alipatikana kesho yake baada ya kuonwa na babu yake katika njia ya kupita ng'ombe na kutoa taarifa polisi.

"Askari walifika katika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha hayo niliyoyataja huku ukiwa umezungukwa na wadudu mchwa kutoka na maeneo yale ambayo yalikuwa na kichaka,"alisema Kamanda Mwakyoma.

 Alisema kutokana na upelelezi wa awali wa  jeshi la polisi inadaiwa chanzo cha kifo cha binti huyo ni wivu wa kimapenzi ambao hata marehemu kabla hajafikwa na mauti alikuwa akisimulia kwa ndugu zake kutokana na kutishiwa lakini hakutaka kufuata sheria kwa kutoa taarifa kwa jeshi la pilisi mapema.

Katika taarifa nyingine iliyotolewa na jeshi la polisi mkoani Mara ilisema watu watatu ambao walikamatwa hivi karibuni kutokana na kukutwa na mali za mradi wa umwagiliaji wa shamba la Serikali la Bugwema lililopo Musoma vijijini wakisafirilisha kama vyuma chakavu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema watu hao walikamatwa Mei 20 na wananchi wa kijiji cha Bugwema kata ya Bugwema tarafa ya Nyanja wilayani Butiama majira ya saa 2:00 usiku baada ya kuwashuku wakiwa wamepakia vifaa mbalimbali vya mradi huo katika gari namba T 497 BFH roli aina ya Nissan mali ya Ebeneza John mkazi wa jijini Mwanza na kutoa taarifa polisi.

 Alisema baada ya gari hilo kufikishwa kituoani walilifanyia upekuzi na kubaini walikuwa wamebeba vyuma chakavu vya katapira Model 621 huku ikiwa imekatwa vipande vinne, pamoja na Mitungi minne ya gesi ambayo hutumika kwa shughuli za umwagiliaji za kijiji hicho
.

Post a Comment