0

 

 KATIBU Mkuu wa Mabingwa wa Soka  Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako, leo amemtambulisha rasmi Mshambuliaji mwenye mapenzi ya moyoni na timu hiyo  Mrisho Ngassa, aliyekuwa na mahasimu wao wakuu, Simba.

Mwalusako, amemtambulisha Ngassa kuwa hivi sasa ni mchezaji mpya na halali wa Yanga, baada ya kuanguka saini ya kuitumikia Klabu hiyo kwa miaka miwili, ili kuisaidia katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara na michuano ya kimataifa, inayoikabili timu hiyo baada ya kuwa mabingwa na Ligi Kuu iliyomalizika jana.
 
Ngassa, ameamua kurudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo na kutimkia, Azam FC na baade kabla ya mwaka jana kuuzwa kwa mkopo, Simba, ambako amekuwa akisumbuliwa kila mara na viongozi hadi mashabiki kuwa hana mapenzi na timu hiyo na hasa kwa kitendo chake cha kubusu Jezi ya Yanga aliyorushiwa na mmoja wa mashabiki wa Yanga, katika moja ya mechi za mwaka jana wakati akiwa Azam.

Aidha Mwalusako, alisema kuwa Ngassa,  ni mchezaji wa kwanza kutangazwa na klabu hiyo na kusani mkataba wa miaka miwili ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu, ambapo ni leo ni siku muhimu iliyokuwa ikisubiriwa na Viongozi wa Yanga, Ngassa na hata mashabiki wa Yanga, waliokuwa wakiushauri uongozi kumrejesha Ngassa ''Tunduni''.  na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.
Ngassa, akibusu Jezi ya Yanga, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Yanga,  Lawrance Mwalusako, wakati wa utambulisho rasmi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment