0
Umoja wa wafanyabiashara wa Usafirishaji mkoani Mara wamelalamikia kitendo cha Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA)mkoa wa Mara kwa ukiukwaji wa sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya Mamlaka hiyo kwa kuruhusu na kupangia safari magari ambayo hayana leseni ya kusafirisha abiria.

Katika barua yao iliyoandikwa kwenda kwa Meneja wa SUMATRA mkoa wa Mara ambayo ilidai inashangazwa na Mamlaka hiyo kukiuka sheria ambazo inazisimamia kwa kuruhusu mambo ambayo yanakwenda kinyume cha utaratibu kwa kuruhusu magari hayo na hivyo kuwanyonya wenye leseni halali.

Barua hiyo ilisema  kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilalamikia suala hilo kwa kufikisha taarifa maeneo husika lakini hakuna hatua zozote ambazo zimekwisha kuchukuliwa na Mamlaka yoyote kutokana na ukiukwaji wa sheria.

 Barua hiyo iliitaka Sumatra mkoa wa Mara ichukue hatua za haraka katika kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa sheria kwa kuwa vitendo vinavyofanyika vina wanyonya wamiliki wengine ambao wanalipa mapato yote kwa mujibu wa sheria za usafirishaji.

 Akizungumzia malalamiko hayo,Meneja wa Sumatra mkoa wa Mara Michael Rogers alikili kuwepo kwa gari lililotajwa namba zake likifanya kazi bila kufuata utaratibu na tayari ameshawasiliana na vyombo vingine vya usalama kufatilia malalamiko hayo.

Amedai gari namba T 930 BVW Toyota Costa leo asubuhi amelikuta likiwa limebeba abiria maeneo ya Musoma Mjini tayari kuelekea Majita Busekera Wilaya ya Musoma Vijijini likiwa halina stika za Sumatra wala bima na kuliamulu kushusha abiria mbele ya polisi.

Post a Comment