0SERIKALI  inakusudia    kuboresha huduma ya maji ili wananchi mkoani Mara  waweze  kupata huduma hiyo kwa uhakika na kuondoa kero ambazo mbalimbali za huduma hiyo ikiwemo umbali wa kupata maji.

 Hayo yalisemwa na Waziri wa  Maji Profesa Jumanne Maghembe akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani humo katika kukagua miradi mbalimbali ya maji.

Alisema  Serikali   imekusudia  kutumia sh.bilioni 1.1  kuboresha  huduma hiyo kwa  kurekebisha  na kununua pampu mpya  kwa kuweka vioski 30  na  miradi kutengenezwa upya kwa kulingana  na watu ili maji yaweze kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao.

Waziri Maghembe alisema  Wizara  ya maji itatumia jumla ya  shilingi Bilioni 300 katika kutekeleza miradi wa huduma ya maji katika mikoa mitatu ya Bukoba ,Mwanza na Mara .

Alisema maeneo ya miradi hiyo ya maji yamesha andaliwa kutokana na mazingira ya mikoa hiyo lengo likiwa kuondoa kero ambazo wanazipata Wananchi kutokana na upatikanaji wa maji.

”Tayari  Wizara yangu imekubaliana  na Benki ya Maendeleo  na kusaini  kuchukua mkopo wa shilingi bilioni 25 ili  kuboresha mradi wa Mgango  uliopo wilaya ya Butiama ambapo katika mradi wa chanzo kipya cha Bukanga  wa wilaya ya Musoma utagharimu shilingi bilioni 80 ”,alisema Maghembe.


Alisema ifikapo mwezi Julai Wizara itakuwa  imeleta wataalam ambao wataangaalia namna  ujenzi wa mIradi hiyo ili kuweza kudumu kwa muda mrefu zaidi  na kufikia miaka 20  kwa mujibu wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi.

Maghembe aliwataka Wananchi  kutoa ushirikiano  kwa wataalam  ili kuharakisha  huduma hiyo inapaikana na kwamba wananchi hao  wakae mkao  wa kupata huduma ya maji ya uhakika.

”Pale ambapo maji yanachukuliwa na kupita ni lazima watu wa eneo hilo wapate maji ili  waweze kusaidia kulinda mradi husika ili wale wasio wazalendo na waharibifu wa miundombinu wasiihujumu”aliongeza.

Akiwa katika Wilaya ya Butiama,Waziri Maghembe alipokea kero za Wananchi kupitia  Afisa Mtendaji wa Kata ya Butiama  Raphael Kakwaya alizitaja kero  zinazosababisha  wananchi kutokupata maji wilayani humo ni mitambo  chavu, baadhi ya watu wanapata huduma hiyo kuwauzia maji kwa bei ya juu  kuanzia shilingi 150 hadi 200 kwa ndoo ya lita 20 na  na wafanyakazi wa Mugango-Kiabakari na Butiama kutolipwa mishahara yao tangu mwaka 2011 na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi .

Waziri wa maji Profesa Maghembe katika  ziara yake   mkoani Mara lengo ni kutembelea na kukagua  miradi  ya maji  kwa kukagua mradi wa Chanzo kipya  cha Bukanga katika wilaya Musoma, mradi wa maji wa Mugango ,Butiama pamoja na kukagua mradi wa bwawa la Manchira Wilayani Serengeti. 

Post a Comment