0
NA IMMACULATE   MAKILIKA- MAELEZO
SERIKALI imesema kuwa itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi nafasi yake katika jamii  kufuatia  kuwepo kwa watu wachache wasiyoitakia  mema nchi  yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano, mauaji  nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati  akitoa kauli ya Serikali  kuhusu mlipuko wa uliotokea katika kanisa la katoliki la Mtakatifu Joseph  Parokia ya Olasiti  Arusha  mjini Mei 5, mwaka huu saa 4:30  asubuhi na kusababisha  vifo vya watu wawili na kujeruhi  59, kati ya hao watatu ni mahututi.

 Aliwataja watu waliofariki dunia kuwa ni Regina Kurusei mwenye wa miaka 45 mkazi wa Olasiti ambaye alifariki siku ya tukio wakati alipokuwa kipatiwa matibabu  katika hospitali ya Mount  Meru na James  Gabriel(16) aliyefariki usiku wa  kuamkia leo.

“Tutachukua hatua kali bila huruma  kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua  hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa  letu kwanza,” alisema Waziri Nchimbi.

 Alisema tayari kikosi kazi maalumu  kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo.
 Waziri Nchimbi alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa  mlipuko huo ni bomu. Hivyo uchunguzi wa kubaini  aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .

“ Hadi  sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambroce mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,mkazi wa Mrombo, Arusha,ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. 
Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wane wa kigeni  na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa maahojiano,” alisema.

 Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali inamewataka wanasiasa  na viongozi wote wajiepushe na kauli zinazochochea  ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongoni mwa Watanzania.

”Serikali isilaumiwe kwa  hatua kali za kisheria itakazozichukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania,” alisisitiza huku akisema Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hilo wanasakwa popote walipo  na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali anaungana na Watanzania kulaani wahusika wote  wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Pia inawataka viongozi  wa kisiasa, kidini,na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Mlipuko huo ulitokea muda  mfupi   baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla. Aidha alikuwepo mwenyeji wake Askofu Josephat  Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha.

Inakadriw a kuwa katika uzinduzi huo kulikuwa na watu zaidi 2000. Hivyo wakati mgeni rasmi akiwa ametoka nje akijiandaa  kukata utepe  kama ishara ya uzinduzi  mtu aalirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa.

Katika tukio hilo viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria ibada hiyo hawakupata

Post a Comment