0WAKAZI Mji wa Musoma na Vitongoji vyake ijumaa hii watapata ladha ya burudani ya muziki wa dansi kutoka kundi zima la Extra Bongo'Next Level chini ya Ally Choki ikiwa ni burudani ya kwanza ya dansi mjini hapa tangu kuanza kwa mwaka huu.

Akizungumzia maandalizi ya unyesho hilo kwa njia ya simu,Mkurugenzi wa Kampuni ya Respect Entertainment ambao ndio waandaaji wa onyesho hilo Muhamed Kiumbe maarufu kama Chief Kiumbe alisema kila kitu kinakwenda vizuri kuhusiana na onyesho hilo na litafanyika kama lilivyopangwa.

Alisema katika onyesho hilo wanamuziki wote wa kundi hilo watakuwepo kuhakikisha wakazi wa Musoma wanapata burudani ya kutosha ambayo itakidhi nafsi na tayari kundi limeshaelekea Musoma.

Chief kiumbe alisema kwa muda mrefu wakazi wa musoma hawajapata burudani ya muziki wa dansi hivyo ameamua wakati kundi hilo likiwa katika ziara ya kanda ya ziwa ni vyema likafika musoma ili liweze kutoa burudani katika mji huo.

"Unajua Musoma ni nyumbani sasa lazima burudani ya viwango ifanyike huko pia na ndio maana nikaongea na Ally Choki aweze kwenda na kikosi kizima cha Xxtra Bongo mjini Musoma ili kuweza kukata kiu ya burudani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kundi hilo la Extra Bongo,Ally Choki alisema wakazi wa Musoma watarajie kupata burudani ya ukweli kwa kuwa kabla ya kuanza ziara ya Kanda ya Ziwa wamefanya maandalizi ya kuhakikisha wanafanya kweli katika ziara nzima.

Choki alisema katika ziara hiyo watatoa burudani ya nyimbo za zamani zilizopatwa kuimbwa na bendi hiyo lakini pia nyimbo mpya kama Mtenda Akitendewa,Ufisadi wa Mapenzi,Farsafa ya Maisha na Mkaribishe Mgeni zitachukua nafasi yake.

Post a Comment