MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHADEMA WILFRED LWAKATARE APATA DHAMANA
HATIMAYE
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Wilfred Muganyizi Lwakatare aamepata dhamana na kurudi uraiani,
baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko
wazi.
Akiwa
katika viwanja vya Hahakama hiyo anasema kwamba, Lwakatare amepata
dhama hiyo yenye dhamani ya tsh 10milioni pamoja na kuwa na wadhamini
wawili wanaotambulika na kukabidhi hati za kusafiria Mahakamani hapo.
Awali
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati
yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai, katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kula njama na kupanga kumteka Dennis
Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu.
Hata
hivyo, Mei 8, mwaka huu Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu aliwafutia
mashtaka hayo matatu ya ugaidi na kuwabakizia shtaka moja linaloangukia
kwenye jinai ya kula njama za kutenda kosa la kumdhuru Msacky kwa
kutumia sumu.
Post a Comment
0 comments