0




Mnyange atakaye uwakilisha mkoa wa Mara katika mashindano ya lake zone na baadae miss Tanzania 2013 anatarajiwa kupatikana usiku wa leo katika ukumbi wa Musoma Club ulipo katikati ya Mji wa Musoma huku shindano hilo likitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila mremmbo kujiandaa.

Jumla ya warembo 20 watapanda jukwaani kuwania taji hilo huku muuandaji wa shindano hilo kutoka kampuni ya Homeland Entertainment Godson Mkama akitamba kwa kusema kuwa anaamini mrembo wa mkoa wa Mara ndiye atakayevaa taji la miss Tanzania 2013/2014.

Akizungumza na BLOG hii Mkama amesema hakuna kitu kitakachokwamisha mrembio kutoka mkoa wa mara kuchukua taji hilo kwani wanazo sifa ambazo zitawafanya kuuwakilisha vyema mkoa wa Mara katika mashindano ya kanda na baadae mashindano ya Taifa.

Amesema katika shindano la mwaka huu kuna tegemewa kuwa na ushindani mkubwa baada ya warembo wengi kuchukua fomu kwa ajili ya ushiriki wa shindano hilo baada ya kupata nafasi za juu katikaka mashindano ya urembo ya Wilaya ambayo yamemalizika hivi karibuni.

Mkama alisema katika shindano la kumsaka mrembo wa miss Tarime kulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa washiriki walioshiriki shindano hilo hivyo kulazimika kuchukua washiriki watano ili waweze kushiriki shindano la mkoa.

"Muitikio umekuwa mkubwa katika shindano la mwaka huu maana warembo wengi wamejiamini na kujitokeza kushiriki mara baada ya kupata taarifa juu ya shindano hili hivyo ni matarajio yangu Redds miss Mara mwaka 20013 litakuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo.

"Serengeti pia kulikuwa na ushindani mkubwa katika kinyang'anyoro cha shindano la  Wilaya ambapo tumechukua washindi wa kwanza hadi wa tatu ambao wataingia kambini kwa ajili ya kushiriki shindano la mkoa ambalo litafanyika juni 7 Manispaa ya Musoma,"alisema Mkama.

 Aidha Mkama ameishukuru BLOG hii kwa kuwa mstari wambele katika kuhamasisha shindano la miss Mara na kuwaomba wadau wengine kuwa pamoja pale linapoandaliwa shindano ili kuweza kuutangaza vyema mkoa kupitia shughuli za urembo

 

Post a Comment