HALIMASHAURI ya Wilaya ya Butiama imevuta kasi
katika kampeni ya kuchangia damu iliyoanza aprili 15 ikiwa na lengo la kuokoa
vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga wakati wa kujifungua.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
uchangiaji wa damu uliofanyika katika viwanja vya mwenge Wilayani hapa,Makamu
Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Musoma Denis Ekwabi alisema hadi
kufikia sasa tayari zimekwisha kusanywa chupa za damu 871 kutoka kwa Wananchi
waliojitolea.
Alisema kiasi hicho cha damu kimekusanywa
kutokana na uhamasishaji uliofanywa na timu ya wakusanya damu kutoka Idara ya
afya chini ya Mganga mkuu wa Wilaya Gencwele Makenge kwa kupita katika maeneo
mbalimbali ya Wilaya.
Ekwabi alisema Wananchi wa Wilaya ya Butiama
wameitikia wito wa uchangiaji wa damu kutokana na kuelewa namna ambavyo vifo
vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga vinatokea wakati wa kujifungua
huku tatizo kubwa linalosababisha vifo hivyo likiwa ni damu.
Alisema kiasi cha chupa 871 za damu ambazo
zimekusanywa hadi sasa ni zaidi ya lengo ambalo limewekwa na mkoa wa Mara
kukusanya chupa 600 kwa kila Wilaya itakapofikia juni 14 siku ya maazimisho ya
uchangiaji damu anbapo kitaifa itafanyika mkoani Mara.
Aidha Ekwabi ameendelea kutoa wito kwa Wananchi
wa Wilaya ya Butiama kuendelea kuchangia damu kwa kuwa hitaji la damu halina
kikomo hivyo kushilikiana na timu ya ukusanyaji damu ili kupata chupa nyingi
zaidi kutoka kwa wale wenye sifa za kutoa.
Awali
mkurugenzi wa Shirika la (Evidence For Action) Craig Ferla linaloshughulika na
kampeni ya uchangiaji wa damu Tanzania alisema vifo vya akina mama na watoto
wachanga wakati wa kujifungua ni vingi hapa Nchini kuliko sehemu nyingine
Duniani hivyo wanaweza kuokolewa kwa kuchangia damu.
Alisema kiasi cha chupa 450,000 za damu
zinahitajika kwa mwaka Nchini Tanzania huku kiasi kikubwa kikitumika kuokoa
maisha ya mama na watoto lakini cha kusikitisha chupa 150,000 za damu ndizo
zinazopatikana na kusambazwa hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika
kuchangia.
"Kiwango kikubwa cha uhaba wa damu
kinapelekea akina mama wengi kufa,takwimu zinaonyesha kina mama 48,000 na
watoto 8,000 ufariki dunia kutokana na upungufu wa damu hapa Tanzania,kiwango
hiki ni kikubwa hivyo lazima tushirikiane kuokoa hali hii.
"Akina mama na watoto wachanga ufariki dunia
kutokana na hali hii,ni lazima kwa pamoja tuhakikishe vituo vya tiba vitoe
huduma stahiki kwa mama zetu na watoto wachanga ili kuwaokoa,"alisema
Craig.
Post a Comment
0 comments