Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh.
Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Na Father Kidevu, Dodoma
Wanafunzi wa Chuo Kikuu
ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za
makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu,
Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.
Pia wameahidi kujichangisha
fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika.
Kauli hiyo ya kwanza
kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku
nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi nla wanafunzi hao walipofika
kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo
muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
“Mimi ninayofuraha
kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu,
baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale
Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa
mwaka wa kwanza hapo UDOM.
“Wewe ni jembe, kama
uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2,
ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii”
mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye
salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.
Lowasa wakati akiwa
waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais
Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili
kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo
kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.
Kwa sasa shule hizo
zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha
na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.
“Mimi ninawashangaa
watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa.
Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha”
alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.
Wanafunzi hao wa UDOM
waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote
nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini
anapata elimu.
Kwa kuanzia wanafunzi
hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo
baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
Kwa upande wake, Lowasa
ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga,
mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko
Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka
wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye
binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza an
galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.
Post a Comment
0 comments