Bw Joseph Mtalemwa -Menaja wa Tigo kanda ya Ziwa alipokuwa akitoa salamu katika maazimisho ya uchangiaji damu ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Mara. |
Bw Joseph Mtalemwa -Menaja wa Tigo kanda ya Ziwa |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na blog hii,walidai katika makampuni ya simu hapa Nchini Tigo imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kutoa mchango katika kulijenga Taifa.
Kutokana hamasa ambayo tigo ilishiriki katika uchangiaji wa damu ilipoelekea mkoa wa Mara kuvuka lengo la makusanyo ya damu katika mkoa ambapo naibu Waziri wa Afya alipozungumza na blog hii baada ya kilele cha maazimisho ya uchangiaji damu alitaka makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni ya Tigo katika kushiriki katika shughuli za kijamii.
soma makala ya damu
KILA tarehe 14 juni
Dunia inaazimisha siku ya wachangia damu duniani(World Blood Donor Day) ikiwa
na lengo la kuwashukuru na kuwatambua wale wote ambao kwa kuelewa umuhimu wa
damu salama huwa wanajitolea kuchangia damu kwa hiari.
Jamii inahimizwa
kuchangia damu ili kuokoa vifo hususani vya mama wajawazito na watoto wachanga
vinavyotokea wakati wa kujifungua huku tatizo kubwa la vifo hivyo ikitajwa kuwa
ni damu.
Takwimu zinaonyesha
kina mama 48,000 na watoto 8,000 ufariki dunia kutokana na upungufu wa damu
hapa Tanzania,kiwango ambacho ni kikubwa kuliko nchi yoyote duniani kwa mujibu
wa wataalamu wa afya.
Kiasi cha chupa
450,000 za damu zinahitajika kwa mwaka Nchini Tanzania huku kiasi kikubwa
kikitumika kuokoa maisha ya mama na watoto lakini cha kusikitisha chupa 150,000
za damu ndizo zinazopatikana na kusambazwa.
Kwa mujibu wa takwimu
za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha jumla ya damu zinazotolewa kila
mwaka ulimwenguni kwa utaratibu wa kujitolea ni chupa milioni 80.
Katika idadi hiyo
niliyoitaja nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hutoa asilimia 38 tu idadi
ambayo haiendani na asilimia 82 ya wagonjwa ambao tiba yao ina uhitaji wa damu.
Imebainishwa wagonjwa
wenye uhitaji wa damu kwa wingi ni watoto chini ya miaka mitano,wanawake
wajawazito,watu wanaopata ajali pamoja na wale wenye magonjwa mbalimbali
yanayosababisha upungufu wa damu.
Tunaweza kuokoa vifo
vinavyotokana na upungufu wa damu kwa kujitoa kuchangia damu kwani kitendo cha
kuchangia damu ni kitendo cha kibinadamu kwani kinaokoa maisha ya binadamu.
Damu salama maana
yake ni ile damu ambayo haina vimelea vya maradhi ambayo yanaweza kuambukiza
mtu mwingine iwapo mtu huyo ataongezewa.
Maradhi ambayo
yametajwa na kuweza kuambukiza kupitia kwenye damu ni Ukimwi (HIV),Homa ya Ini
(Hepatitis) pamoja na Kaswende (Syphilis) ambayo yanachunguzwa na vituo vya
damu salama vilivyopo kila kanda.
Majukumu makuu ya
vituo vya damu salama vinatakiwa kuhakikisha malengo ya upatikanaji wa damu
salama yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kutoa uhamasishaji kwa jamii ili kuweza
kuchangia.
Lakini licha ya
kuhamasisha jamii kujitoa kuchangia damu kitu muhimu kinachopaswa kufanywa na
vituo vya damu salama ni kuhakikisha damu inapimwa kwa usahihi na kwa utaalamu
wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama wake.
Nikirejea katika
suala la kuchangia watu wengi hawatambui umuhimu wa kujitolea kuchangia damu
katika kuokoa maisha ya binadamu ili hatimaye kila mtu mwenye afya nzuri awe
mchangiaji damu wa mara kwa mara.
Katika uzinduzi wa
kampeni ya kuchangia damu mkoani Mara iliyofanyika Wilayani Bunda,mkurugenzi wa
Shirika la (Evidence For Action) Craig Ferla linaloshughulika na kampeni ya
uchangiaji wa damu Tanzania alisema vifo vya akina mama na watoto wachanga
wakati wa kujifungua ni vingi hapa Nchini kuliko sehemu nyingine Duniani hivyo
wanaweza kuokolewa kwa kuchangia damu.
Post a Comment
0 comments