JESHI
la polisi mkoani Mara linawasaka Wanawake wawili ambao wanadaiwa
kuwatelekeza kwa kuwatupa watoto wawili wachanga katika matukio
mawili tofauti yaliyotokea katika Manispaa ya Musoma.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari ofisini kwake,Kamanda wa polisi mkoani Mara
Ferdinand Mtui alisema jeshi la polisi bado linaendelea kumsaka Mwanamke
mmoja ambaye alitelekeza mtoto wake mchanga wa kiume mwenye umri wa
siku mbili juni 24 maeneo ya Bweri na kuokotwa na dereva wa bodaboda.
Katika
tukio hilo,dereva wa pikipiki huyo aliyetambulika kwa jina la
PeterPhinias Mkazi wa Rwamlimi akiwa katika mizunguko yake alimuokota
mtoto huyo akiwa ndani ya shimo huku akiwa hai.
Alisema
baada ya kumuokota alimpeleka katika kituo cha polisi kati Musoma na
muda mfupi baada ya kuokotwa mtoto huyo mama mmoja aitwaye Kulwa Julius
alijitokeza na kudai mtoto huyo ni mjukuu wake na kumkabdhi kwa ajili ya
matunzo zaidi huku Jeshi la polisi likiendelea kumtafuta Mwanamke
aliyetupa mtoto huyo.
Katika tukio lingine,Kamanda Mtui alisema mnamo julai 3 majira ya saa 6 mchana maeneo ya kambi ya polisi (FFU) Musoma
aliokotwa mtoto
anayesadikiwa kuwa na umri wa mwezi mmoja mwenye jinsia ya kike.
Alisema
mtoto huyo alitelekezwa nyuma ya nyumba ya askari polisi na mtu ama
watu wasiojulikana na kugunduliwa a wapita njia ambao walitoa taarifa
jeshi la polisi na kwenda kumchukua eneo la tukio.
Mtui
alisema bada ya mtoto huyo kuchukuliwa
alipelekwa kituo cha polisi baadae kupelekwa hospitali ya Serikali ya
mkoa wa Mara kwa lengo la kuangaliwa afya yake pamoja na hifadhi.
Kamanda
wa polisi mkoani Mara alidai uchunguzi wa kina bado unaendelea kubaini
mzazi wa mtoto huyo na kuweza kufikishwa katika vyombo vya seria huku
akitoa wito kwa yoyote mwenye taarifa juu ya wazazi hao aweze kuitoa.
Aidha
kamanda Mtui alisema jeshi la polisi katika kipindi cha mwezi mmoja
kimekamata makosa 120 yakiwemo ya kuvunja nyumba usiku na
kuiba,kupatikana na mali inayodaiwa ya wizi,kupatikana na nyara za
Serikali,madawa ya kulevya pamoja na wizi wa mifugo.
Alisema
makosa hayo yalipatikana baada ya kuendesha msako katika Wilaya ya
Musoma,Serengeti,Bunda na Butiama na kufanikiwa kupatikana wahalifu wa
makosa mbalimbali wapatao sitini na tatu (63).
Post a Comment
0 comments