MBUNGE WA JIMBO LA RORYA LAMECK AIRO AKIKAGUA UJENZI WA MRADI WA BWAWA LA MAJI KATIKA KIJIJI CHA OSIRI KATA YA ROCHE |
Wananchi
wa Kijiji cha Osiri kilichopo Kata ya Roche wilayani Rorya wanalazimika
kwenda maeneo ya Nchi jirani ya kenya kwa ajili ya kupata huduma ya
maji kwa
mahitaji mbalimbali hali iliyowafanya kumuomba Mbunge wa jimbo hilo
Lameck Airo kusaidia kukamilika kwa mradi wa maji wa Tasaf ulioanzishwa
kijijini hapo.
Hayo
wameeleza mbele ya Mbunge huyo alipokuwa akikagua miradi mbalimbali ya
Maendeleo
katika Jimbo la Rorya na kudai kutokana na uhaba wa maji kunawapelekea
kuvuka mipaka hadi Nchini kenya kwa ajili ya kupata maji kwa ajili ya
matumizi ya binadamu pamoja na wanyama.
Walisema
tatizo la maji katika kijiji hicho na vijiji vingine vitatu vilivyopo
Kata ya Roche kunawasababishia kuishi katika mazingira magumu ya kukosa
huduma hiyo ikiwemo kwa binadamu pamoja na wanyama wanaowafunga.
Wananchi
hao waliishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi wa bwawa la maji kupitia
mradi wa Tasaf lakini wakaomba nguvu ya Mbunge wa Jimbo hilo ili uweze
kukamilika kwa haraka na ufanisi zaidi ili kuondokana na adha hiyo.
"Tunaishukuru
sana Serikali kwa mradi huu wa maji hapa Osiri kwani tuna matatizo
makubwa sana lakini kutokana na nguvu zetu pia tunaomba na nguvu za
Mbunge wetu ili mradi huu ukamilike mapema nasi tupate maji.
"Kwa
sasa tunalazimika kwenda kupata huduma ya maji Nchi jirani ya Kenya kwa
ajili ya matumizi ya binadamu pamoja na mifugo yetu na sio karibu na
hapa kijijini hivyo tunaangaika kupata huduma hiyo,"alisema Onyango
Samwer.
Akizungumza
mara baada ya kuangalia mradi huo,Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo
alisema atakuwa bega kwa bega kuhakikisha mradi huo unakamilka kwa
kuweka nguvu zake na
kuongeza vifaa ili uweze kukamilika.
Alisema
amewasiliana na mkandarasi wa Halimashauri na kumtaka wakandarasi
waliopo katika eneo la mradi waweze kukaa eneo hilo hadi mradi
utakapokamilika na yupo tayari kughalamikia ziada ya mradi huo.
"Nimeagiza maroli yangu yaje hapa na yatafika hapa ili kuweza
kusaidia shughuli za hapa na maji yaweze kupatikana ili adha ya matatizo ya maji mliyonayo yaweze kukamilika kwa muda muafaka.
"Naomba
nanyi Wananchi muwape ushirikiano wakandarasi kwa kile watakachowaleza
ili mradi huu usije kuaribika kwa kuingilia eneo la mradi kwa kilimo na
shughuli nyingine ambazo zitakwamisha,"alisema Lameck.
Post a Comment
0 comments