Akitoa
malalamiko yake hivi karibuni kwa Waandishi wa Habari Mjini Bunda,Marwa
alidai licha ya kuwasilisha malalamiko yake kwa wakati tofauti
katika ofisi mbalimbali za serikali bado maofisa wa aridhi waliovamia
maeneo yake wameendelea kuyashikilia huku wakiwa wamejenga nyumba zao na
kukahidi maelekezo yaliyotolewa.
Alitaja
ofisi alizowahi kuwasilisha kero zake kuwa pamoja na Ofisi ya mkuu
wilaya ya Bunda, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Baraza la ardhi, nyumba
na Makazi mkoani Mara na Kamishna ya Ardhi Wizarani lakini bado maamuzi
hayafanyiwi kazi huku akiendelea kuangaika kuitafuta haki yake ya kurudishiwa maeneo.
Akionesha
vielelezo kwa Wandishi wa Habari, alisema Mahakama ya Ardhi, Nyumba na
Makazi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara ilihukumu kesi hiyo MISC
Application No.85 ya mwaka 2010, kwa kutoa siku 30 kwa maofisa wa ardhi
kumrejeshea eneo lake katika Kitongoji cha mashine ya maji mjini humo.
Alisema
agizo lilitolewa Novemba 5, 2010 ambapo Kampuni ya UBAPA LTD and
Tribunal Broker ilitakiwa kubomoa nyumba zilizojengwa katika eneo lake
lakini anashangazwa na kampuni kuendelea kuwa na kigugumizi cha
kutekeleza agizo lililotolewa huku akidai huenda kampuni hiyo inashindwa
kufanya hivyo kwa kuwa inategemea kazi nyingi kutoka katika idara ya
ardhi ya Bunda.
Vielelezo
vimebaini kuwa hiyo ni hukumu ya pili ambapo hukumu ya kwanza ya
kurejeshewa eneo lake lilitolewa na Baraza la ardhi la Kata ya Bunda
Na.77 mwaka 2009 lakini Ofisa ardhi ya wilaya ya Bunda wakati huo (jina
tunalo ) hakuridhika na kukata rufaa kuhamisha hukumu hiyo kwenda
mahakama ya ardhi nyumba na makazi wilayani Musoma.
Kutokana
na hatua hiyo April 4, mwaka huu Mahakama ya Ardhi Nyumba na Makazi
Musoma iliagiza Kampuni ya UBAPA and TRIBUNAL BROKER kutekeleza agizo la Mahakama hiyo Na.85 ya mwaka 2010.
Marwa
alidai kwamba kwa muda huo wote, maofisa hao wanatumia fedha
ili agizo la mahakama hiyo isitekelezwe huku wakiendeleza eneo hilo
licha ya kuzuiliwa na badala yake waliamua kumfikisha polisi kuwa ni
mvamizi na kudai anasikitishwa na na anavyofanyiwa licha ya kuwa na umri
mkubwa na kuviomba vyombo vya juu kumsaidia kuipata haki yake ambayo
anadai vielelezo vyote anavyo huku akikabidhi nakala ya vielelezo hivyo
katika Gazeti hili ikiwemo barua kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.
Post a Comment
0 comments