MKUU
wa mkoa wa Mara John Tupa amewahimiza viongozi
kuanzia ngazi za Kata,Wilaya na mkoa kuhakikisha wanasimamia na kuwa na
ufatiliaji wa karibu kuhakikisha mifugo inaogeshwa ili kuweza kuepukana
na magonjwa yanayotokana na kupe na kusababisha vifo vya mifugo.
Kauli
hiyo ameitoa wakati wa kikao cha majumuisho ya mradi wa ufufuaji wa
majosho ya kuogeshea ng'ombe uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uholanzi (SNV) kwa kushirikiana na wadau wa mifugo mkoani Mara.
Amesema
kazi kubwa iliyofanywa na SNV na wadau wa mifugo kwa kufatilia ufufuaji
wa majosho kwa lengo la kuhakikisha mifugo inaogeshwa inafaa kuenziwa
kwa viongozi kutoa elimu kwa wafuagaji nakuona umuhimu wa kuogesha
mifugo ili kuwaepusha na magonjwa yaenezwayo na kupe.
Tupa
ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema mkoa wa Mara ambao una
mifugo mingi zikiwemo ng'omb zaidi ya milioni moja ambayo Wananchi
wamekuwa wakitumia kama uchumi,chakula na mahitaji mengine inafaa
wafugaji wapate elimu ya kutosha namna ya
kufuga kwa tija na utamaduni wa kuosha mifugo.
Amesema
kila Wilaya lazima ijue uhitaji wa majosho katika maeneo yao na kutumia
ongezeko
kubwa la majosho lililopo kutokana na kazi iliyofanywa na SNV na wadau
wa mifugo wafugaji waweze kuogesha mifugo na kutokomeza vifo ambavyo ni
zaidi ya asilimia 70 vinavyotokana na ugonjwa unaosababishwa na kupe.
Amesema
ruzuku ya dawa inayopatikana kwa mkoa wa Mara haiendani na idadi ya
mifugo hivyo ni muhimu ruzuku hiyo ikaongezwa ili
kuendana na hali halisi pamoja na Serikali ya mkoa wa Mara kuvumbua
njia ya mifungo inapopita kwenda kuoshwa kutokana na maeneo mengine
kuvamiwa na wakulima.
Kwa
upande wake Meneja wa mradi wa mifugo kutoka Kanisa la Anglican
dayosisis ya Mara (AIC-Mara)ambao walishirikiana na SNV dokta Theophil
Kayombo amesema baada ya kutembelea mjosho katika kufatilia ufufuaji
wamekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutotekelezwa kwa sheria
ndogo ndogo za ogeshwaji wa mifugo.
Amesema
Serikali inapaswa kuweka mkazo katika uogeshaji wa mifugo kutokana na
baadhi ya Wananchi kuwa na visingizio vingi pale wanaposhindwa kwenda
kuogesha mifugo na kuwa na mawasiliano kutoka ngazi ya josho ili kuwza
kufatilia uogeshaji.
Post a Comment
0 comments