CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini kimejipanga kwa kuanza ziara
ya kutembelea kata 13 za Wilaya hiyo kuwakumbusha viongozi
na wanachama wake wajibu wao katika Chama lengo likiwa kujiimalisha na
kuweka nguu ya pamoja kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja ya kukijenga
chama na kufanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo
mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza
na MTANZANIA mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea kata hizo
iliyoongozwa na Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM (NEC) Vedastus
Mathayo,Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini Musa Motoroka alisema ziara
hiyo ni moja ya majukumu ya Chama katika kukumbushana wajibu na
utendaji wa kazi.
Alisema
ziara hiyo ilikuwa na mafanikio kwa kukutana na viongozi na wanachama
wa kutosha na kuzungumza nao mambo mbalimbali ambayo
yana lengo la kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisa kazi za Chama kuanzia
ngazi za Tawi,Shina hadi Kata zinafanywa kwa ushirikiano kwa kusudio
moja la kukijenga Chama.
Katibu
huyo wa CCM alisema bila kuwa na vikao na kukumbushana wajibu wa
majukumu ya kila mmoja kama Chama cha Siasa kazi haziwezi kwenda na kila
mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake akiwa kiongozi ama mwanachama kwa
kushiriki shughuli zote ikiwa katika Shina,Tawi ama Kata.
"Tumefanya
ziara katika Kata zote 13 za Wilaya yetu ya Musoma Mjini na imekuwa na
mafanikio makubwa kwa kukutana na viongozi wote pamoja na wanachama na
kupanga mambo mbalimbali na kuhimizana kila mmoja kutimiza wajibu wake
akiwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.
"Ziara
hii sio ya kwanza,tunakutana na viongozi na wanachama wetu mara kwa
mara katika kukumbushana wajibu,unajua mbeleni kuna uchaguzi wa Serikali
za Mitaa kwa hiiyo siri kubwa ya ushindi ni kuwa pamoja na kufanya
vikao na ndio
maana tunafanya ziara katika kukumbushana wajibu,"alisema Motoroka.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM (NEC) Vedastus Mathayo
alisema ahadi yake ya kuzifanya ofisi zote za CCM Musoma Mjini kuwa za
kisasa kwa kuzitengeneza imeshaanza kwa kuwakumbusha viongozi wa Kata
kuharakisha kutafuta maeneo ambayo yatajengwa ofisi hizo.
Alisema
ahadi yake aliyoitoa katika uchaguzi ndani ya CCM ataitekeleza mara
moja iwapo viongozi wa Kata watampelekea mapendekezo yao mahala ambapo
wanataka ofisi yao ikae na kudai kuwa alitoa ahadi hiyo kwa kuamini
shughuli za Chama zinapaswa kufanyika mahala ambapo ni pazuri na sahihi.
Post a Comment
0 comments