TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Mara
(TAKUKURU) inamshikiria askari wa jeshi
la polisi mkoani mara namba F.1863 Maridad David Kapinga wa kituo kikuu cha
polisi mjini Musoma kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya shilingi elfu
ishilini.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari,Mkuu wa Takukukuru
mkoa wa Mara Holle Makungu alisema
askari huyo mnamo septemba 10 mwaka huu alikamatwa na maafisa wa Taakukuru
akipokea kiasi hicho cha fedha baada ya kumuomba kiasi hicho cha fedha Raia
mwema na kutoa taarifa Takukuru.
Alisema askari huyo aliomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa
mtu huyo baada ya kufatilia kitambulisho chake
cha mkazi alichomdhamini ndugu yake kama masharti ya dhamana aliyekuwa
na tuhuma zilizofunguliwa katika kituo hicho kwa kumbukumbu RB/2818/2013.
Holle alisema baada ya kupokea taarifa hizo mtego uliwekwa
ili kuweza kumnasa askari huyo ambapo maafisa wa Takukuru walifanikiwa
kumkamata askari huyo maeneo ya Tanesco Musoma akiwa tayari ameshapokea kiasi
hicho cha fedha.
Mkuu huyo wa Takukuru alisema uchunguzi dhidi ya tukio hilo
bado unaendelea kufanywa na Taasisi hiyo na mara utakapokamilika hatua zaidi
zitachukuliwa kwa askari huyo kwa mujibu wa sheria zinazozuia vitendo vya
kuchukua na kupokea Rushwa.
Alisema askari pamoja na watumishi wa Umma kwa ujumla wao wana kila sababu kuzingatia
maadili ya kazi zao katika utekelezaji wa nyadhifa walizokabidhiwa na kuepukana
na kuomba Rushwa kwani kufanya hivyo kunapelekea haki stahili kupotea na
kukwamisha shughuli za kimaendeleo.
Aliongeza kuwa maafisa wa Takukuru wataendelea kutekeleza
majukumu yao kwa kuwafatlia wale wote wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa na
kudai kazi hiyo haiwezi kufanikiwa bila kuwa na ushirikiano baina ya Wananchi na na wale wote wanaochukia vitendo
vya Rushwa.
Aidha Holle amewaasa
Wananchi mkoni Mara kuendelea kutoa taarifa kwa taasisi hiyo ili kuweza
kukomesha vitendo vya kuomba na kupokea Rushwa vinavyofanywa na watumishi
katika idara mbalimbali ambao sio waaminifu.
Post a Comment
0 comments