MWANAFUNZI mmoja wa kidato cha pili katika shule ya
sekondari Mukendo Masejo Mashanshu (19) amefariki dunia akitibiwa
katika hospitali ya Mkoa wa Mara,baada ya kuchomwa kisu na kujeruhiwa vibaya
sehemu ya ubavuni na kijana mwenzake ambaye akuweza kufahamika mpaka sasa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa
wa Mara Ferdinand Mtui alisema mnamo septemba 17mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika maeneo ya Rwamlimi mjini hapa marehemu alichomwa kisu na kijana mwenzake na kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubavuni upande
wa kulia hali iliyompelekea kuvuja damu nyingi na kupelekea kupoteza maisha akiwa kwenye matibabu.
Alisema baada ya kujeruhiwa alifikishwa kituo cha polisi na kupewa
PF.3. lakini ilipotimu majira ya saa mbili usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa
matibabu katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Kamanda Mtui
alisema chanzo cha tukio hilo bado alijafahamika na hakuna mtu yeyote
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo,na kusisitiza kuwa jeshi la polisi
linaendelea kumsaka mtu aliyehusika na
tukio hilo na mara atakapopatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi
Mtui alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za
siri kwa jeshi la polisi kuhusiana na tukio
hilo ili kuweza kufanikisha kukamatwa wale wote waliohusika na
kuwatakawanafunzi pale wanapoona viashilia vya kutisha uhai kujiepusha
kwa kukaa mbali na kutoa taarifa jeshi la polisi kama kuna mtu ama watu
wanaotishia uhai.
Post a Comment
1 comments:
Daah vitendo hivyo miaka ya hivi karibun vilipungua kwanini wanataka mauaji yaendelee?