WAMAMA WA LINE POLISI WAKISUBILI MKWANJA
MSIENDE KUSUKIA NYWELE ZA GHARAMA HIZI FEDHA!
MIJIERA LIVE!
TIA SAHIHI HAPA KABLA YA KUPOKEA TUSIJE KUGEUKANA,NI KAMA ANASEMA MTENDAJI WA MUKENDO
MWENYEKITI BI.MWAMVITA ADAMU AKIPOKEA FUNGU TOKA MWAKILISHI WA MBUNGE NYERERE DIWANI WA VITI MAALUMU BI.MARIAMU(CHADEMA)
NI FURAHA TUPU BAADA YA KUVUKA MKWANJA
KIKUNDI cha
Wanawake wajasiliamali cha Mshikamano Line Polisi kilichopo katika Manispaa ya
Musoma kimeupongeza uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kupitia Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Vicenti Nyerere kwa kufatilia na
kuhakikisha vikundi vya Wanawake na Vijana vinapata mikopo kwa ajili ya
Maendeleo.
Wanawake hao
walisema kwa zaidi ya miaka mitano ya nyuma tangu wamekuwa wakijishughulisha na
ujasiliamali hawajawahi kupata mikopo kutoka Halimashauri ya Manispaa ya Musoma
nah ii ni mara ya kwanza kuona wanatazamwa na kupata mikopo hiyo ambayo
imedaiwa huwa inatoka kila wakati kupitia mfuko wa Maenmdeleo.
Kauli hiyo
ilitolewa na Wanawake hao wanaoishi Kata ya Mukendo baada ya kukabidhiwa kiasi
cha shilingi milioni mbili na laki tatu na Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini na
Diwani wa Kata ya Mukendo Vicenti Nyerere (Chadema)ili kuongeza mitaji kwenye
shughuli zao za ujasiliamali ikiwa ni mikopo ya gharama nafuu na kurudishwa kwa
ajili ya kuwapa watu wengine.
Akizungumza
mara baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha,Mwenyekiti wa kikundi hicho chenye
wanachama 20 Mwamvita Adamu, alishukuru kuona uongozi uliopo sasa kwenye
Manispaa ya Musoma kufatilia na kuhakikisha vikundi vya ujasilimali vinapata
mikopo nafuu inayotoka kwenye mfuko wa Maendeleo hivyo kubolesha na kuimalisha
biashara zao.
Alisema
mikopo waliyopata watahakikisha hawaiweki kwenye shughuli nyingine zaidi ya
kuongeza mitaji ili kuweza kujiongezea kipato na kuweza kuirudisha ili watu
wengi zaidi waweze kukopeshwa na kuondokanana wimbi la umasikini katika
familia.
Mwenyekiti
huyo alisema licha ya kusikia huwa kuna fedha kwenye Halimashauri
zinazokopeshwa kwa gharama nafuu kwa vikundi vya Wanawake na Vijana lakini
hawajawahi kupata fedha hizo na ni mara ya kwanza na kudai uongozi wa sasa
uliopo unapaswa kupongezwa kwa hatua hiyo.
Akizungumza
na Wanawake wa kikundi hicho kabla ya kutoa fedha hizo kwa niaba ya
Mbunge,Diwani wa viti maalumu Mariamu Daud(Chadema) alisema fedha hizo zitatolewa
kwa Kata zote 13 za Jimbo la Musoma na wameanza na Kata ya Mukendo na kusema
fedha zote zitakazo husika na mikopo ya Wanawake na Vijana zinawafikia.
Alisema
katika vikao walivyokaa vya Halimashauri ya Manispaa ya Musoma kwa kushirikiana
na Mkurugenzi na madiwani ni kuhakikisha fedha zinazokuja kwa ajili ya mikopo
ya vikundi vya Wanawake na Vijana kuhakikisha zinawafikia ili kuwawezesha
kuendeleza shughuli zao za ujasilimali na kupata kipato.
Mariamu
alisema kwa sasa hawatakubali kuona fedha zinakuja kwa ajili ya mikopo ya
Wanawake na Vijana kisha zinapelekwa kwenye shughuli nyingine na kuwaacha
Wanawake na Vijana wakiendelea kukosa fedha hizo na kuendelea kuwa masikini.
Awali Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mukendo Roda Laurian alisema ana amini Wanawke hao
hawatashindwa kurejesha fedha hizo kwa kuwa zinalejeshwa baada ya miezi sita
kwa asilimia tano na kuwataka Wanawake hao kuhakikisha fedha hizo wanazitumia
kwa malengo yaliyokusudiwa.
Post a Comment
0 comments